Serikali Kuleta Madaktari Kutoka Nje Ya Nchi - Bilioni 200 Zatengwa Kuwalipa-mbona sielewi hii filamu hivi muongozaji na mtunzi ni nani au ni ya kanumba?.
Posted in
No comments
Sunday, July 1, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Serikali
imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya
wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Habari
kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa
serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana
mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.
Habari
kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia
ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa
kuboresha maslahi yao.
Kwa
mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya
kuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza
limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na
zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari
wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.
Habari
zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki,
zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba
kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.
Inaelezwa
kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu,
madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200
waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa
kazini kwa masharti makali.
Hata hivyo, uamuzi wa serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.
Baadhi
ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada
ya Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo
liko mahakamani.
Mbunge
wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali
ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali
haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi
mahakamani, “Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile
jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati
jambo lipo mahakamani?” alihoji Dkt. Kigwangala.
Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.
Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala
huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Juzi
uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliwafukuza kazi madaktari
229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo
unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :