SHIGONGO AELEZEA SABABU ZA KUSHIKILIA PASSPORT YA JOSE CHAMELEONE.
Posted in
No comments
Sunday, July 29, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Najua watu wengi wametaka
kusikia Mr Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers atazungumza nini
kuhusu kuishikilia passport ya mwimbaji Jose Chameleone wa Uganda.
Kama bado hujaisikia hii ishu,
inabidi ufahamu kwamba kuna ishu inaendelea kati ya watu hao wawili, Big
Boss Eric Shigongo anamdai Chameleone dola elfu 3500 ambazo alilipwa
mwanzoni kabla ya kulipwa dola elfu 8 baadae kwa ajili ya kuja kuperfom
Tanzania kwenye Tamasha la usiku wa matumaini Uwanja wa taifa.
Alikuja kupiga show vizuri kwa
mujibu wa mkataba wa pili aliolipwa dola elfu 8 lakini baada yakumaliza
show, kesho kutwa yake ndio stori ikatoka kwamba Jose Chameleone
kanyang’anywa Passport na Shigongo kwa sababu anamdai dola elfu tatu mia
tano za mwanzo.
Chameleone alisaidiwa kurudi
kwao na ubalozi wa Uganda Tanzania lakini anachosema kuhusu
kunyang’anywa passport ni kwamba hizo pesa hakulipwa yeye bali promota
feki aitwae George huko Kampala Uganda, so Chameleone aliporudi home
alimkamata George na kumepeleka polisi lakini baadae aliachiwa huru.
Juzi Jose Chameleone
aliandamana na watu wake mpaka ubalozi wa Tanzania Uganda akiutaka
ubalozi huo ufanye juu chini apate passport yake anayodai kanyang’anywa
na Eric Shigongo kwa sababu anamdai.
Kabla ya hii ishu kuwa kubwa,
tayari Global Publishers ambao ni waandaaji walishafanya maamuzi mengine
ya busara ya kwenda kwenye Ubalozi wa Uganda hapa Tanzania na kueleza
kilichotokea lakini hawakupata msaada wowote na baadhi ya wafanyakazi wa
ubalozi huo walimfanya mwakilishi wa Global Publishers kupata picha ya
fikra mbaya baada ya wafanyakazi hao wawili kuongea kwa kiganda huku
wakicheka baada ya kupewa hiyo taarifa ya Chameleone kutapeli.
Erick Shigongo amesema “mimi
sisemi kwamba Watanzania tuwe watu wabaya lakini ni vizuri tukajua jinsi
ya kusimamia haki zetu, sisi tumelelewa kwa upole toka wazee wetu huko
nyumba tunarithi tu hiyo kitu”
Kuhusu huyo Promota feki aitwae
George, Shigongo amesema “mimi nilimfahamu George kupitia kwa Kidumu
alieniambia ni mtu pekee anaefanya kazi na wasanii wengi Uganda, Kidumu
alipokwenda Kampala walikutana hawa watu Chameleone akiwa ana haraka
haraka ya kuondoka kwenda kwenye show Sudan, hivyo mbele ya Kidumu
Chameleone akaruhusu huo mkataba usainiwe na George huku Kidumu ndio
akitoa hizo pesa”
Juzi Chameleone alipoandamana
alikua na mabango mbalimbali huku mengine yakiandikwa Erick Shigongo
yuko juu ya sheria kiasi gani mpaka kuishikilia passport yake toka july 9
2012.
Kuhusu ishu ya kuishikilia
Passport ya Chameleone, Shigongo amesema “hakuna mtu anaeshikilia
Passport ya Chameleone isipokua Chameleone alifata utaratibu wa kawaida
kwenye hoteli anapoingia kwa kukabidhi fedha zake na document muhimu na
Hoteli ilikua ni ya kwetu, tulipoanza kumdai tukitaka atulipe kabla
mazungumzo hayajafika mwisho wakati wa mvutano akaondoka bila kuaga
hotelini, hakunyang’anywa passport yake ila aliziacha Reception”
Kuhusu kumchukulia hatua za
kisheria, Shigongo amesema “kuna mambo mawili yatafanyika kwa sababu
nilipokutana na uongozi wa Wizara ya mambo ya nchi za nje waliniomba
nirudishe Passport ili watumie njia za kidiplomasia kuhakikisha nalipwa
pesa zangu, hiyo ni option ya kwanza… ya pili tunawasiliana na
wanasheria wetu ili kuona namna gani tunaweza kushughulikia hili swala”
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :