REDD'S MISS KANDA YA KASKAZINI JUMAMOSI HII NAURA SPRING
Posted in
No comments
Tuesday, September 4, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
WAREMBO
11 wameingia kambini juzi Jijini Arusha kujifua kwaajili ya shindano la
Redd’s Miss Kanda ya Kaskazini 2012, linalotaraji kufanyika jumamosi
Septemba 8, 2012 jijini Arusha.
Warembo
hao watapanda jukwaani katika Hoteli ya Naura Spring mjini humo kuwania
taji hilo linalo shikiliwa na mrembo Stacy Alfred ambaye alinyakua taji
la Mrembo mwenye Haiba ya Picha (Miss Photogenic 2011) katika Shindano
la Miss Tanzania 2011.
Mwandaaji
wa shindano hilo kupitia kampuni ya Jazz Promotions, Emma Mroso amesema
kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yanakwenda vyema na warembo wapo
katika afya njema.
Aidha
Mroso amewataja warembo walioingia kambini na wanaendelea na mazoezi
yao kuwa ni Mishi Mziray, Dalina Hashim, Anita Mboya, Highmanna Lyimo,
Anande Radhiel, Waridi Frenk, Buya Ernest, Lucy Stephano, Neyla Hashim,
Trovina Mpanda na Theresia Kimolo.
Mratibu
huyo amesema kuwa warembo hao walistaili kuwa 12 ikiwa ni warembo 3
kila mkoa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga ispokuwa
mshiriki mmoja Sara Benjamin anaumwa na yupo Nairobi kwa matibabu.
Shindano
hilo linataraji kupambwa na burudani kali kutoka kwa Banan Zoro na
kundi zima la B Band pamoja na wasanii wengine mbalimbali wa jijini
Arusha.
Shindano la Redd’s Miss Kanda ya kaskazini 2012 limedhaminiwa na Redd’s
Original, Dodoma Wine, Naura Springs Hotel, Brazil Lounge, Father
kidevu Blog, Modern holdings EA ltd, Honeys furniture, Little Roses,
Jazz collection, Camro Insurance Services, Eannaso, Anyor
Designs, Triple A FM, Ndeku hair salon, Compumania celltronics,TLK
investments, Computer and Secretarial College, Arusha Art, Cyber Net,
Riverside Shuttle, eo security na Authentic Emergency Services.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako


0 MAOINI :