CHEKA ATWAA UBINGWA WA IBF AFRIKA-JIJINI ARUSHA
Posted in
No comments
Thursday, December 27, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo na rais wa TPBC Onesmo Ngowi wakimvisha mkanda Francis Cheka |
Baada ya Mpambano kumalizika Cheka allisema anashukuru ameshinda ila mpambano ulikuwa mgumu sana kwake na alikiri hajakutana na bondia mkali kama Chimwemwe kwa karibuni.
Francis Cheka akiongea na waandishi wa Habari baada ya pambano kumalizika |
Majaji wa pambano hilo ambao walikuwa watatu walitoa maksi kama ifuatavyo: David Chikwanje alimpa Cheka pointi 112/114 za Chimwemwe, Boniface Wambura alimpa Cheka pointi 118/114 za Chimwemwe na James Ligongo alimpa Cheka pointi 120/115 za Chimwemwe
Frincis Cheka akikwepa konde la Chimwemwe |
Cheka ameweza kutwaa Ubingwa wa IBF Afrika baada ya kunyang'anywa kwa kushindwa kuutetea kwa muda na akaenda kucheza na Karama Nyilawila ubingwa wa UBO ambao pia alimpiga Nyilawila.
Naye Meya wa jijini la Arusha Gaudence Lyimo alimpongeza promota wa pambano hilo Andrew George na Rais wa TPBC Onesmo Ngowi kwa kuleta pambano hilo la kimataifa Arusha na kusema atashirikiana nao kuwahakikisha anainua mchezo wa ngumi Arusha.
Jaji Boniface Wambura akitafakari kitu kabla mpambano kuanza |
"Nawapongeza walioleta pambano hili Arusha na wnawaahidi tutakuwa tukishirikiana bega kwa bega kuahakikisha tunainua mchezo wa ngumi Arusha", alisema Meya. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :