MBUNGE BETTY MACHANGU AIPONDA SERA MWANAMKE AKIWEZESHWA ANAWEZA
Posted in
No comments
Monday, December 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
MBUNGE wa viti maalum CCM Mkoa Wa Kilimanjaro, ambaye pia ni
mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Betty Machangu amewataka wanawake
kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi katika jamii na kijitambua
ili kuondokana na dhana ya mwanamke bila kuwezeshwa hawezi.
Machangu aliyasema hayo katika ziara ya kutembelea wilaya
sita za mkoa wa Kilimanjaro, kujionea juhudi zinazofanywa na vikundi vya akina
mama katika ngazi ya tarafa ambapo aliwataka wanawake kujitambua, kujiwezesha
na kukataa msemo wa mwanamke akiwezeshwa anaweza.
Alisema dhana ya kwamba mwanamke ni mtu wa kutegemea
kuwezeshwa na mwanamme ni ukatili wa kijinsia na uonevu na kuwataka akina mama
kusimama kwa kujiamini ikiwa ni pamoja na kutambua nafasi waliyonayo kama
walezi katika jamii.
“Wanawake sasaifike muda tujitambue na kukataa kauli hii ya
kwamba mwanamke hawezi mpaka awezeshwe, huu ni udhalilishaji na ukatili wa
kijinsia, wanawake tujishughulishe badala ya kusubiri kwezeshwa, uwezo tunao,”
alisema Machangu.
Sambamba na Ziara hiyo, Mbunge huyo alitoa Semina ya
ujasiriamali kwa wanawake na jinsi ya kubuni biashara mpya na siyo kusuibiri
fedha za matumizi kutoka kwa waume zao na kuongeza kuwa kufanya hicvyo kila
mwanamke atajikomboa kutokana na udhalilishaji na kwamba hiyo ndiyo njia pekee
ya kuondokana na mfume dume.
“Kuna fursa nyingi tu za biashara, mwanamke kinachotakiwa ni
kuwa mbunifu na sio kukaa nyumbani kufanywa magoli kipa kila siku, kama
tutajitambua naamini, matukio ya udhalilishaji na unyanyasaji yatapata dawa,
mwanamke hoyee!!” alisema.
Katika semina hiyo wanawake
kutoka katika wilaya za Same, Moshi, Hai, Siha na Mwanga walifundishwa kubuni
miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo walibuni miradi ya mbuzi wa maziwa,
Nguruwe, Kuku wa mayai na Nyama, ambayo
waliona wanaweza kufanya na kujiingizia kipato.
Aidha akiahidi kuchangia katika miradi hiyo, Machangu alisema
kuwa, wanawake wengi wamejisahau na
kujijengea ile dhana ya kuwa mwanamke
hawezi kuongoza sekta zinazoongozwa na mwanamme kama kuongoza nchi na
kusisitiza haja ya wanawake kujitambua uwezo wao ikiwa ni pamoja na kujiamini
kuwa wanaweza.
MWISHO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :