MISA TAKATIFU YA MAZIKO YA ASKOFU AMEDEUS MSARIKIE MOSHI; RAIS KIKWETE KUHUDHURIA
Posted in
No comments
Thursday, February 14, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
M
|
isa
Takatifu ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi Amedeus
Msarikie inaendelea katika Kanisa la Kristo Mfalme Moshi mkoani Kilimanjaro.
Misa ya Leo inaongozwa na Baba Askofu
Tarsisius Ngalalekumtwa ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Taarifa
iliyotolewa na Uongozi wa Kanisa hilo imesema majira ya saa 7: 30 mchana huu
kutafanyika Maziko katika Kanisa la Kristo Mfalme Moshi ambapo Mwili wa
Marehemu Amadeus Msarikie utazikwa.
Ibada hiyo ya maziko
itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kanisa, viongozi wa Kisiasa nchini,
Viongozi wakuu wa Serikali wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Viongozi mbalimbali ulimwenguni
wametoa salamu zao za rambirambi kufuatia msiba huo mkubwa wa Kanisa Katoliki
akiwemo Balozi wa Papa nchini Tanzania.
Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa
mwaka 2012 Marehemu Askofu Amedeus Msarikie aligundulika kuwa na ugonjwa wa
saratani na mwanzoni mwaka huu alipelekwa Mjini Nairobi kwa ajili ya matibabu ambapo
alifariki Februari 7 akiwa na umri wa miaka 82.
Baba Askofu Ngalalekumtwa
ametaja Marehemu Msarikie kama kiongozi wa kuigwa ambaye aliwekeza katika elimu
pia miaka 52 aliitumia katika Upadre na miaka 27 katika nafasi ya Uaskofu ndani
ya kanisa hilo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :