Dkt. Mukangala aagiza RT kufuta Uteja katika Riadha

Posted in
No comments
Sunday, March 3, 2013 By danielmjema.blogspot.com


 WAZIRI wa Michezo Habari na Utamaduni Dk. Fenela Mukangala ameziagiza Chama cha Riadha nchini (RT) na kamati ya Maandalizi ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon kuhakikisha wanaweka mipango mikakati ya kufuta uteja wa wanariadha wa Tanzania kwa nchi jirani ya Kenya.

Agizo hilo kutoka kwa Waziri huyo mwenye dhamana ya Michezo imekuja baada ya Wakenya, Kipsang Kipkemoi (2:14:56), Julius Kilimo (2:15:44) na Dominic Kiagor (2:16:25) wakitawala nafasi za mwanzo huku hali kama hiyo ikijitokeza katika mbio za kilomita 42 upande wa wanawake ambayo ilishuhudia nafasi ya kwanza akichukua, Edna Joseph (2:39:05), nafasi ya pili, Eunice Muchiri (2:41:00) na nafasi ya tatu akichukua mkenya mwengine, Frida Too (2:44:04).
mbio za kilomita 42 katika eneo la kuanzia- uwanja wa ushirika Moshi
 Dk. Mukangara Ameyasema hayo jana katika Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Mjini Hapa na kushuhudia wakenya wakiendeleza ubabe wao katika mbio hizo kama ilivyokuwa mwaka jana na miaka iliyotangulia.
 Dk Mukangala hata hivyo alimpongeza Mtanzania wa pekee aliyeibuka mshindi kwa kuwabwaga wakenya kawenye mbio za kilomita 21, Sarah Makera aliyetumia nmuda wa saa 1:13:05 kumaliza mbio hizo na kumwacha Mkenya Vicory Chepkemoi (1:14:34), akipigania nafasi ya pili na Mtanzania aliyeshika nafasi ya Tatu, Faituma Matanga (1:15:35).

Dk. Mukangala akisalimiana na mshindi wa kwanza wanawake, Sarah mbio za kilomita 21
Waziri amesema kuwa lengo la mashindano lisiwe tu kuandaa bali kuwa mshiriki na sio msindikizaji kama ilivyo sasa ambapo Wanariadha wa Tanzania wamekuwa wasinndikizaji tu.

"Lengo la kuandaa mashinedano haya yasiishie tu katika hatua ya Maandalizi, tusishiriki kama wasindikizaji tu, tuingie katika mashindano kama wapambanaji na lengo liwe ni kushinda, Watanzania dwamechoshwa bna uteja wa Wakenya ifike mahala Waandaji tufikirie njia za kubadilisha hali hii," amesema Dk.Mukangala.

kwa upande wake Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka amesema kuwa maandalizi ya mbio za mwaka zimefana sana huku akibainisha kuwa kamati ya utendaji RT inajipanga kukutana kuangalia namana ya kurekebisha makosa na kufuta uteja kwa Kenya katika Riadha.

Rais wa RT-Bwana Anthony Mtaka
Mtaka amesema kuwa katika miaka ya Nyuma enzi za wakimbiaji kama Jumaa Ikangaa, Filbert Bayi, Wilhelm Gidabuday, Steven John Akhwari mabo yalikuwa tofauti na kuongeza kuwa RT imeshaanza kufanya mikakati ya kuhakikisha kuwa inaandaa wanariadha tangu wakiwa wadogo kwa kutambua vipaji na kuvikuza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema kuwa kufanyika kwa mbio hizo katika ardhi ya kilimanjaro hasa mji wa Moshi ni fursa kubwa na heshimakubwa ambayo haitakiwi kufanyiwa uzembe wa aina yoyote ile.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
Gama amesema kuwa uwepo wa mbio za kilimanjaro marathon katika mji huu imesaidia sana kukuza uchumi wa mji na pamoja na uchumi wa mkoa na kuongeza kuwa kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa maandalizi ya wakimbiaji katika miaka ijayo inazingatiwa.

Katika mbio za mwaka huu ambazo huratibiwa kila mwaka na kampuni ya Executive Solution, Wild Frontiers na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kwa kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager zimeshuhudiwa washiriki zaidi ya 6500 kutoka katika kila kona ya dunia akiwemo Kocha wa Timu ya Taifa,Taifa Stars, Kim Poulsen aliyeshiriki mbio za kilomita 21.


wadhamini wengine ni Gapco (mbio za walemavu), Vodacom (kilomita 5 fun run), TPC, Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet na Kilimanjaro Water, Marenga Investment.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .