MAKUNDI MKOMBOZI CUP YAPANGWA, BINGWA MTETEZI KUUMANA NA GREEN STAR

Posted in
No comments
Wednesday, June 12, 2013 By danielmjema.blogspot.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bingwa Mtetezi wa Kikombe cha Mkombozi Kitayosce FC atafungua michuano hiyo kwa kucheza na Green Star zote za mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkombozi Cup michuano hiyo itaendeshwa kwa makundi, ambapo kundi A lina Bingwa Mtetezi Kitayosce FC, Green Star, Nyuki FC na Golani FC.

Mechi ya Ufunguzi imepangwa kuchezwa Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa Mandela, Kata ya Pasua Mjini Moshi.

Kundi B lina Kili Rangers, Mvuleni, Nazareth na Soweto. Kundi C lina TPC, New Generation FC, Best Maridadi FC na Moshi UTD. Kundi D limeundwa aa ajili ya mashindano hayo vimtolewa kwa timu zote ikiwemo mipira na jezi.

Mwenyekiti wa Mashindano haya Mama Mshana amewataka wadau wa soka wilayani Moshi kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano ya kuinua vipaji wilayani humu.

Mkombozi Cup itatia nanga Julai 8 mwaka huu, na viwanja vya King George Memorial na Mandela vitatumika, kwa timu 16 kuchuana vikali kumpata Bingwa wa Mkombozi Cup 2013.

MAKUNDI YA MKOMBOZI CUP 2013 KATIKA JEDWALI


MKOMBOZI CUP 2013


KUNDI A
KUNDI B
KUNDI C
KUNDI D
1
KITAYOSCE
KILI RANGERS
TPC
RELI
2
GREEN STAR
MVULENI
NEW GENERATION
SANGO
3
NYUKI FC
NAZARETI
BEST MARIDADI
KILI FC
4
GOLANI FC
SOWETO FC
MOSHI UTP
BOYS UTD

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .