MTANZANIA MWENYE UMRI WA MIAKA 14 ANAYETENGENEZA APPLICATION ZA SIMU NA KUWAUZIA NOKIA
Posted in
No comments
Saturday, June 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa
Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini Singapore. Akiwa na umri wa
miaka 14 na mwanafunzi wa kidato cha pili huko Singapore, tayari
ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya wataalamu wa application
katika moja ya makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononi
ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications ambazo anazituma katika
kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia. Kwa idhini ya mama yake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Walter P. Makundi,
ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Singapore siku
alipokutana na kuzungumza nao.
Bw. Makundi, ambaye ni Meneja mradi wa
kampuni kubwa ya ujenzi ya APCO PTE LTD ya hapo Singapore, ndiye baba
mzazi wa Alvin. Kulia kwake ni mkewe, Mama Alvin.
Chini Rais Kikwete akisalimiana na Alvin ambaye aliongozana na mama yake pamoja na dada kuja kumuaga wakati Rais akiondoka Singapore usiku huu.
CHANZO:CHUMA BLOG
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :