ATLETICO MINEIRO MABINGWA WAPYA WA COPA LIBERTADORES!
Posted in
No comments
Thursday, July 25, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
WAKIWA kwao, Estádio Governador
Magalhães, huko Belo Horizonte, Brazil, Atletico Mineiro, walipindua
kpigo cha 2-0 toka Mechi ya kwanza na Alfajiri hii ya Leo kuifunga
Olimpia Bao 2-0 na kutwaa Ubingwa wa Copa Libertadores,
Klabu Bingwa ya Marekani ya Kusini, kwa Mikwaju ya Penati 4-3 baada
Mechi kwenda Dakika 120 na Matokeo kubaki 2-0 na hivyo Jumla ya Magoli
kuwa 2-2.
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0
huku Olimpia wakiutumia vyema Mfumo wao wa Kidifensi, 5-3-2, kwa
kujihami sana na kuiacha Atletico wakitawala.
MAGOLI: Atletico Mineiro 2 -Dakika ya 46 Jô -87 Leonardo Silva
Lakini Kipindi cha Pili Atletico Mineiro
walicharuka na kufunga Bao zao 2 na kuifanya Mechi iwe Sare kwa Jumla
ya Magoli 2-2 kwa Mechi mbili na hivyo kwenda Dakika za Nyongeza 30
ambazo hazikutoa Mshindi.
Olimpia walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 85 baada ya Manzur kupokea Kadi ya Njano ya pili na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Baada Dakika 120 ikaja Tombola ya
Mikwaju ya Penati na Atletico Mineiro ikaibuka kidedea kwa Penati 4-3
baada ya wao kufunga Penati zao zote 4 na Olimpia kukosa mbili
zilizopigwa na Miranda na Gimenez.
PENATI:
Atletico Mineiro 4-Alecsandro-Guilherme-Jô-Leonardo Silva
Olimpia 3
-Miranda [ALIKOSA]-Ferreyra-Candia-Aranda-Gimenez [ALIKOSA]
VIKOSI:
ATLETICO MINEIRO [Mfumo 4-2-3-1]: Victor, Michel, Réver, Leo Silva, Júnior César, Pierre, Josue, Tardelli, Ronaldinho, Bernard, Jo
Akiba: Rosinei, Guilherme, Alecsandro, Gilberto Silva, Leandro Donizete, Lee, Luan
OLIMPIA [Mfumo 5-3-2]: Silva, Mazacotte, Manzur, Miranda, Candia, Benitez, Pittoni, Aranda, Silva, Salgueiro, Bareiro
Akiba: Gimenez, Baez, Ferreyra, Meza, Paredes, Hermosilla, Castorino
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :