Bartoli Bingwa Mpya Wimbledon!

Posted in
No comments
Sunday, July 7, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Marion Bartoli of France holds her trophy, the Venus Rosewater Dish, after defeating Sabine Lisicki of Germany in their women's singles final tennis match at the Wimbledon Tennis Championships, in London July 6, 2013. REUTERS/Stefan Wermuth (BRITAIN - Tags: SPORT TENNIS TPX IMAGES OF THE DAY)
bingwa mpya wa Wimbledon upande wa wanawake-Marion Bartoli
Bingwa wa mchezo wa tennis kwa wanawake katika mashindano ya Wimbledon Marion Bartoli amesisitiza kuwa namna alivyocheza siku ya Jumamosi(06.07.2013) huenda ni mwanzo wa ukurasa wa mafanikio yake katika mchezo huo. 

Bartoli alipata ushindi wake wa kwanza wa Grand Slam siku ya Jumamosi wakati Mfaransa huyo alipofanikiwa kumshinda Sabine Lisicki kutoka Ujerumani kwa seti 2-0 , 6-1 na 6-4 katika fainali ya Wimbledon.
Marion Bartoli of France (R) embraces Sabine Lisicki of Germany after defeating her in their women's singles final tennis match at the Wimbledon Tennis Championships, in London July 6, 2013. REUTERS/Toby Melville (BRITAIN - Tags: SPORT TENNIS) Marion Bartoli
Bartoli mwenye umri wa miaka 28, ambaye alishindwa na Venus Williams katika fainali iliyopita ya Grand Slam ya Wimbledon mwaka 2007 , ni mwanamke wa tano mwenye umri mkubwa kiasi kuwa mshindi kwa mara ya kwanza wa mashindano makubwa.
Aendelea kutabasamu
Kwa upande wake Sabine Lisicki kama kawaida yake alikuwa akitabasamu huku akikiri kuwa alikuwa na wasi wasi mwingi kabla na wakati wa mchezo na kupoteza mchezo huo muhimu kwake na kwa Ujerumani kwa jumla.

Mjerumani huyo alionekana wazi kuwa fainali yake ya kwanza ya Wimbledon ilikuwa ngumu na alionekana dhahiri kuwa alikuwa anaelekea kupata kipigo cha kudhalilisha cha huenda 6-1 na 6-1. Lakini aliweza kupata ushindi katika michezo mitano mfululizo na kurejesha hali ya heshima .
Marion Bartoli of France (L) holds her trophy, the Venus Rosewater Dish, after defeating Sabine Lisicki of Germany (R) in their women's singles final tennis match at the Wimbledon Tennis Championships, in London July 6, 2013. REUTERS/Toby Melville (BRITAIN - Tags: SPORT TENNIS) Wimbledon-Finale in London Marion Bartoli Sabine Lisicki 
 
Alibubujikwa na machozi uwanjani wakati akicheza seti ya pili na kujikuta akishindwa lakini alijikusanya upya kabla ya kuukabili umma wa mashabiki waliokusanyika uwanjani hapo na vyombo vya habari mbali mbali vya dunia.

Lisicki alimshinda bingwa mtetezi Serena Williams na makamu bingwa wa mwaka jana Agnieszka Radwanska katika njia yake kuelekea katika fainali, na alipigiwa upatu kumshinda Bartoli aliyeko katika nafasi ya 15 ya orodha ya wachezaji bora duniani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .