El Baradei kuwa waziri mkuu wa Muda, Misri

Posted in
No comments
Sunday, July 7, 2013 By danielmjema.blogspot.com



Kiongozi mkuu mwenye siasa za  wastani Mohammed El Baradei anatarajiwa kutangazwa kama waziri mkuu wa mpito nchini Misri. 

El Baradei ni mkuu wa zamani wa shirika la masuala ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa na pia mwanaharakati wa Upinzani. 

Kwa  mujibu  wa  shirika la habari la  taifa  Al Mena, Baradei hapo jana alikutana na rais wa muda Adly Mansoor. 

Hata hivyo hatua ya Mohammed Baradei kupewa cheo cha waziri mkuu imezua maandamano makubwa kutoka kwa wafuasi wa rais aliyepinduliwa madarakani Mohammed Mursi.

Huku hayo yakiarifiwa hapo jana rais wa Marekani Barack Obama amesema nchi yake haiungi mkono chama chochote cha kisiasa nchini Misri wala kundi lolote. Obama amelaani ghasia zinazoendelea katika maeneo tofauti nchini humo. 

Siku ya Ijumaa wafuasi wa Mursi pamoja na wapinzani wake walikabiliana vikali na kusababisha  vifo vya watu 35 huku zaidi ya 1000 wakiwa wamejeruhiwa. 

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .