BULEMBO: "VIBOKO KATIKA SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI CCM NI LAZIMA"

Posted in
No comments
Sunday, July 21, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu, Hai

Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) na mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa, Abdallah Bulembo ameagiza kuendeleza adhabu ya viboko kwa wanafunzi wote wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi kote nchini  ili kurudisha nidhamu mashuleni.


Bulembo aliyasema hayo jana wakati akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wari iliyoko katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, na kusema kuwa suala la viboko katika shule za wazazi ni lazima. 

Alisema malezi kwa vijana hivi sasa yameporomoko kutokana na wazazi kutowajibika ipasavyo hali ambayo imemesababisha vijana wengi kutowaheshimu walimu, na hata wakati mwingine mzazi amekuwa akidiriki kumwadhibu mwalimu eti kisa kampiga mtoto wake.

“Suala la viboko kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za wazazi lazima ili kumweka katika malezi mazuri maana hata sisi tulichapwa viboko ndiyo maana leo hii mnapotuona hapa ni kutokana na malezi tuliyolelewa na wazazi wetu na ndio maana tumefika hapa tulipo hivi sasa”alisema Bulembo.

Alisena sisi wazazi tumnasema huwezi kuendelea kuwalea wanafunzi kama ambavyo wazazi wao wanavyotaka, na kama mzazi anaona kuwa mwanae hawezi kuchapwa viboko amwondoe hapa.

Aidha bulembo aliongeza kwa kusema kuwa wapo baadhi ya wanafunzi hawalipi ada na akatoa agizo kwa  wanafunzi wote ambao hawajalipa karo ya shule kuondoka katika maeneo ya shule hizo ili kutafuta shule ambazo zinapokea wanafunzi wasiokuwa na ada.

“Katika hili nitakuwa mkali kweli mwanafunzi, asiyelipa ada aanze kufungasha mizigo yake akatafute shule ambayo wanasoma bure, Walimu wanofundisha wakiwa hawajalipwa nmishahaara wamekuwa wakija makao makuu, kwa nini leo hii mwanafunzi anayesoma hapa asilipe ada? Alisema.

Bulembo yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kukagua uhai wa chama na jumuiya zake sambamba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .