MIRUNGI (MIRAA) KUPIGWA MARUFUKU UINGEREZA
Posted in
No comments
Thursday, July 4, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mmea unaotumika sana na
unaoaminika kulewesha, Miraa au Khat , huenda ukapigwa marufuku nchini
Uingereza kinyume na ushauri uliotolewa na baraza la kuchunguza matumizi
mabaya ya madawa ya kulevya AMCD.
Mwezi Januari, baraza hilo lilisema kuwa Miraa
haistahili kuharamishwa kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha
unaathiri afya ya watu.Uamuzi wa Uingereza kuchukua hatua hiyo unazingatia zaidi usalama na masharti ya kimataifa, hasa kuwa Uingereza inaweza kutumika kama kivukio cha mmema huo kuelekea katika nchi zingine za Ulaya.
''Ikiwa tutakosa kuchukua hatua kubadilisha sheria kwa upande wa Uingereza , huenda ikatishia nchi hii kwa sababu huenda ikatumika kama kivukio,'' alisema Bi May katika taarifa yake.
Lakini wanaharakati wanasema kuwa wamekasirishwa na hatua ya serikali kukosa kutilia maanani ushauri wa baraza lilaloshughulikia maswala ya utumizi mbaya wa madawa ya kulevya.Khat hutumiwa na jamii za wasomalia, watu kutoka Yemen na Ethiopia.
Wizara ya mambo ya ndani ilisema kuwa mmea huo unalewesha kidogo kuliko madawa mengine ingawa baraza la kudhibiti utumizi mbaya wa madawa ya kulevya ilisema kuwa haikupata ushahidi wowote kuwa mmea huo unalewesha.
Makundi ya wasomali nchini Uingereza yaliambia baraza la AMCD kuwa Miraa husababisha matatizo makubwa ya kijamii na kusema inaleta matatizo ya kiafya na kuathiri familia nyingi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :