Mzozo wa familia ya Mandela watokota
Posted in
No comments
Thursday, July 4, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mjuu wake Nelson Mandela, Mandla
, amewatuhumu jamaa zake kuwa na njama ya kutaka udhibiti wa mali ya
babu yake rais wa zamani wa Afrika Kusini.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, yungali hali mahututi hospitalini lakini madaktari wamedhibiti hali yake.Rais Jacob Zuma alitoa taarifa baada ya kumtembelea mzee Mandela hospitalini mjini Pretoria.Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya familia ya Mandela juu ya urithi wake lakini imekithiri huku hali yake ya kiafya ikiendelea kuwa mbaya zaidi.
Mzozo huu wa hivi karibuni kuhusu makaburi unatokana na hoja ya wapi azikwe Mandela akifariki.Stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani wiki jana zilionyesha kuwa anatumia mashine ya kupumua.Alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi Juni baada ya kuugua maradhi ya mapafu.
Mkewe amesema kuwa Mandela wakati mwingine anasumbuka lakini hajalalamika kusema anahisi uchungu wowote.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :