POULSEN ASISITIZA KASEJA BADO NI TANZANIA ONE

Posted in
No comments
Wednesday, July 3, 2013 By danielmjema.blogspot.com


Siku kadhaa baada ya klabu yake ya Simba kutangaza kumtema mchezaji wa mkongwe Juma Kaseja, kocha wa timu wa timu ya taifa ya Tanzania Mdenmark Kim Poulsen ametangaza kikosi cha timu ya taifa na kumjumisha Kaseja ndani ya kikosi hicho.

Poulsen akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho kinachojiandaa na michuano ya CHAN  na kiporo cha mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia, alisema amekuwa akisoma na kusoma sana habari zinamhusu Kaseja na klabu yake kupitia kwenye vyombo vya habari, lakini yeye kwa upande wake amesema bado anamuamini Kaseja na ataendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi chake: 

"Nimekuwa nikisikia taarifa nyingi zinamhusu nahodha wetu Juma Kaseja, ningependa kuweka suala hili wazi kwamba Kaseja bado ni mchezaji mzuri na anafanya kazi nzuri sana ndani ya timu ya taifa. 
 
Ni nahodha mzuri kwa sababu ni kiongozi mzuri kwa wenzie nje na ndani ya uwanja. Hivyo kwangu hali itaendelea kuwa vile vile na nategemea kesho kumuona akijiunga na kambi ya timu ya taifa, ataendelea kuwa nahodha na pia golikipa namba 1 wa kikosi changu.
 
 Kuhusu yeye na klabu yake nisingependa kuyaingilia, lakini kwangu Kaseja bado ni muhimu kwa sababu amekuwa akifanya nzuri kwenye timu ya taifa. Kuhusu hatma ya huko mbele, tusubiri muda utaongea," alisema Kim Poulsen.

Wachezaji wengine walioitwa kwenye timu ya Taifa ni kama ifuatavyo: 

Makipa 
Juma Kaseja 
Ally Mustapha
Mwadini Ally
Aishi Mwanula.

Mabeki
Aggrey Morris
Kevin Yondani
Canavaro
Shoamari Kapombe
Erasto
Vicent
David Luhende

Viungo
Mcha Khamis
Kazimoto
Sure Boy
Domayo
Chanongo
Kiemba

Washambuliaji
Mrisho Ngassa
Simon Msuva
John Bocco
Juma

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .