OBAMA ARUDI MAREKANI AKITOKEA DAR ES SALAAM

Posted in
No comments
Wednesday, July 3, 2013 By danielmjema.blogspot.com



Rais Barack Obama wa Marekani leo amekamilisha ziara yake barani Afrika.Ziara hiyo ameimalizia Tanzania alikowasili hapo juzi ambapo jana asubuhi aliweka shada la maua katika eneo la mripuko wa bomu kwenye ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam.
Obama na Michelle.Mwezi Agosti 1998 Waislamu wenye mafungamano na kundi la Al Qaeda walifanya mashambulizi ya mabomu katika balozi za Marekani mjini Nairobi Kenya na Dar es Salaam Tanzania na kuuwa watu zaidi ya 200. Katika shambulio la Dar es Salaam Watanzania 10 waliuwawa.

 Obama leo hii pia alitembelea mtambo wa umeme ulioko Ubungo mjini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwekeza dola bilioni saba kutanuwa mtandao wa huduma za umeme barani Afrika.

Jana usiku  Obama alikuwa na mazungumzo na viongozi wa biashara.Tayari Rais  huyo wa Marekani ameondoka nchini Tanzania . Awali ilizitembelea pia Senegal na Afrika Kusini.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .