WATAALAMU WATAFUTA MIILI WESTGATE NAIROBI

Posted in
No comments
Thursday, September 26, 2013 By danielmjema.blogspot.com

             Jengo la Westgate Liliporomoka
Vikundi vya maafisa wa uchunguzi wa mauaji vinatafuta miili ya mateka waliouawa ndani ya jengo la Westgate ambao idadi yao haijulikani.
Mateka walizuiliwa na magaidi kwa siku nne kabla ya serikali kutangaza kumalizika rasmi kwa shambulizi hilo
Zaidi ya watu 65 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku amesema kuwa hatarajii kuwa idadi ya waliofariki itaongezeka na kusema kuwa miili ya magaidi pakee ndio itapatikana ndani ya vifusi.

Hii ni baada ya sehemu ya jengo hilo kuporomoka wakati shughuli za uokozi zilikuwa zinaendelea .
Lakini kwa mujibu wa shirika la Red Cross, watu 61 wangali hawajulikani waliko.Wakati huohuo, Kenya inaendelea na siku tatu za maombolezi ya vifo vya raia na baadhi ya maafisa wa usalama waliofariki katika shambulizi hilo.

Mazishi ya mtangazaji mmoja wa Televisheni na Redio, Ruhila Adatia yalifanyika siku ya Alhamisi.
Bendera zingali zinapeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya wale waliofariki.Walinzi walionekana wakichunguza abiria kabla ya kuabiri magari ya usafiri.

Huku wasiwasi ukiongezeka miongoni mwa wakenya kuhusu hali ya kujiandaa kwa maafisa wa usalama kuhusiana na mashambulizi kama haya, taarifa zinasema kuwa serikali inajiandaa kudurusu mikakati yake ya kupigana dhidi ya ugaidi na majanga mengine.

Kundi la kigaidi la Al Shabaab linasema limeshambuli Kenya kutokana na nchi hiyo kujihusisha na vita dhidi ya kundi hilo nchini Somalia

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .