HALI YA KIBINADAMU NI MBAYA JAMHURI YA AFRICA YA KATI (CAR)
Posted in
No comments
Wednesday, October 16, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Waasi wa Seleka wanasemekana kuzua rabsha upya katika maeneo ya Magharibi mwa nchi Shirika la misaada la Medecins
Sans Frontieres (MSF), limesema kuwa maelfu ya watu wamelazimika
kutoroka makwao katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati kutokana na ghasia
zilizoibuka upya.
Wafanyakazi wa afya kutoka katika shirika hilo, wanasema kuwa wanashuhudia visa vya mauaji nchini humo.Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliothirika zaidi na ambao wanatibiwa kwa majeraha ya risasi , panga na silaha zengine za kijadi magharibi mwa nchi.
Wafanyakazi wa mashirika ya misaada pia wamekuwa wakishambuliwa.Vijiji vyote vimeteketezwa na shirika hilo limesema kuwa limepokea visa vya mashambulizi yanayotokana na migawanyiko ya kidini.
Mapigano kati ya makundi ya kutoa ulinzi kwa wanakijiji pamoja na waasi wa zamani yamewalazimisha maelfu kutoroka makwao huku shirika hilo likisema kuwa hali ya kibinadamu sasa ni ya kusikitisha sana na inahitaji kushughulikiwa kwa dharura.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :