MSANII WA UGANDA ALIYEFIA KATIKA SWIMMING POOL AMESAFIRISHWA KWENDA KWAO.

Posted in
No comments
Tuesday, October 22, 2013 By danielmjema.blogspot.com

MacElvis
Mac Elvis alikuja Tanzania wiki mbili zilizopita kwa ajili ya consert Dar es salaam akiwa na wasanii wenzake kutoka Uganda ambao walirudi baada ya consert ila yeye akabaki ili kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Tanzania.

Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake, anasema ‘Alhamisi Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa Lulu (Sio mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni mida ya saa moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu alimwambia asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis aliiamua kuogelea hivyohivyo’

‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati huo Mac akienda kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake kuogelea mara nyingi huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni… Lulu aliporudi hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji huyu ameshaondoka, akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini haikupokelewa’ – Gee
swimming

‘Kesho yake mida ya saa nne mlinzi ndio akaona nguo pembeni na aliposogelea akaona mwili wa Mac ndani ya swimming pool chini ambapo baada ya kutolewa alionekana akiwa na jeraha kwenye paji la uso hivyo inaonekana alijigonga akitaka kujirusha, tumbo lake halikujaa maji kama ambavyo ilidhaniwa, tayari mipango ya kumsafirisha imekamilika na anapelekwa kwao Uganda leo October 22 2013′ – Gee

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .