Rais Banda awafuta kazi mawaziri kwa ufisadi
Posted in
No comments
Friday, October 11, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Bi banda amesema kuwa mawaziri wapya watateuliwa hivi karibuni bila ya kutoa maelezo zaidi.
Aliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kabla kutangaza kulivunja.Kwenye mkutano na waandishi wa habari Banda alisema kuwa ameunda jopo maalum likijumuisha polisi na maafisa wa serikali kufanya ukaguzi wa matumizi ya pesa za serikali katika idara zote za serikali.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kupigwa risasi kwa bwana Mphwiyo ndio ilikuwa mwanzo wa taarfa kuwa baadhi ya maafisa wa serikali wanashirikiana na wafanyabisahara kuifilisi serikali katika utoaji wa kandarasi na mikataba bandia.Washukiwa wanne walikamatwa kuhusiana na kupigwa risasi kwa afisa huyo.Takriban maafisa kumi wa serikali wamaekamatwa wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao kuhusiana na ufisadi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :