DIWANI WA CHADEMA NA WENINE 8 MBARONI KWA KUITAPELI TANESCO KILIMANJARO

Posted in
No comments
Friday, October 11, 2013 By danielmjema.blogspot.com


ACP-Robert Boaz
Mwandishi wetu, Moshi
SIKU chache baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Gharib Mohammed Bilal kuliagiza Shirika la Umme Nchini  Tanesco kuchukua hatua dhidi ya watu watakaobainika kulihujumu shirika hilo, Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kuwakamata watu tisa, akiwemo diwani mmoja wa Chadema, waliohusika na wizi zaidi ya shilingi milioni 169.
Katika Hotuba yake aliyoitoa baada ya kuzindua mradi wa kupoza umme katika kijiji cha Makuyuni wilaya ya Moshi, mkoani hapa, Dkt. Bilal alitoa maagizo ya kuchukua hatua ydhidi ya watu watakaobainika
kushiriki katika wizi wa fedha za umma kwa kulipwa malipo yasiyostahili na kusababisha malalamiko ya kutolipwa watu waliostahili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP- Robert Boaz, alisema kuwa kufuatia agizo hilo, jeshi lake lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika mradi huo, jumla ya watu tisa walilipwa malipo hewa ya shilingi milioni 169,217,000.

Boaz aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Zakayo Reuben Kimathi (52), mkazi wa Mandaka Mnono Saningo, ambaye alilipwa shilingi milioni 10, 342, 000, Elisaria Fredson Mosha (56), ambaye ni Diwani wa kata ya Moshi Magharibi, ambaye alilipwa shilingi milioni 9, 630,000.

Wengine ni Oforo Onsia Kimambo (56), mkazi wa Mandaka Mnono, ambaye alilipwa milioni 29, 000,000 Daudi Narasha Mallya (69) mkazi wa Chekereni, ambaye alilipwa milioni 8, 610, 000, Richard Theretio Mlaki (69), mkazi wa Kiborloni, ambaye alilipwa shilingi milioni 18, 622, 000 na Focus Herman Shayo (88), mkazi wa Kilototoni.

Aidha Boaz alisema kati ya hao Tisa, Jeshi hilo limeshawatia nguvuni watu sita, huku wengine watatu wakiwa hawajapatikana waliko na wakati huohuo likiwashikilia wengine wawili ambao walishiriki kufanikisha wizi huo.

Aliwataja watu hao kuwa ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandaka Mnono, Hassan Awadhi Nduva (41) na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Vendelini Mawazo Shayo (51) na kwamba uchunguzi unaendelea kubaini washiriki wengine katika tuhuma hizo na utakapo kamilika wote watafikishwa Mahakamani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .