TAMKO LA KLABU YA WAANDISHI KILIMANJARO KUHUSU KITENDO CVHA ASKARI MMOJA (JINA TUNALO) KUWAZUIA WAANDISHI WA HABARI KURIPOTI HABARI ZA MAHAKAMA (OCTOBER 2, 2013)
Posted in
No comments
Thursday, October 3, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Uongozi wa Klabu ya waandishi wahabari Kilimanjaro, MECKI,
ulipokea malalamiko ya baadhi ya wanachama wake kuhusu kukinzwa kwa uhuru wao
katika kufuatilia na kuripoti taarifa za kesi mbalimbali kwenye mahakama kuu
mkoa wa Kilimanjaro.
Baada ya kupokea malalamiko hayo, ujumbe wa MECKI
ukimjumlisha mwenyekiti, Bw. Rodrcik Makundi, katibu mtendaji, Bw. Nakajumo
James na mratibu wa Klabu, Bw. Yusuph Mazimu, uliamua kukutana na jeshi la
Polisi kupitia kwa kamanda wa Polisi wa mkoa Kilimanjaro, R. Boaz kujadiliana
Kuhusu kuwepo kwa mazingira yasiyo rafiki kwa waandishi kutekeleza majukumu
yao, yanayodaiwa kuwekwa na Polisi wanaolinda usalama kwenye eneo la mahakama.
Katika kikao hicho kilichofanyika October 1, 2013 katika
ofisi za kamanda Boaz, kilitoka na azimio lifuatalo: Pamoja na kupata kibali
kutoka kwenye mamlaka nyingine ikiwemo mahakama, waandishi wanapaswa
kuwasiliana na “incharge” wa polisi aliyeko mahakamani kwa wakati huo, ili
kutopishana katika kutekeleza majukumu ya kila upande:mahakama, polisi na
waandishi wa habari.
Kuwasiliana na Incharge wa polisi kutawezesha kutotokea kwa
mgongano wa kiutendaji baina ya makundi yote yanayofuatilia kesi, lakini pia
katika kuimarisha ulinzi kama ilivyo majukumu ya jeshi la polisi katika eneo
lolote lile.
MECKI inatambua umuhimu wa kuimarishwa kwa ulinzi katika
maeneo yote na hasa ya mahakama zinapoendelea kesi kubwa kubwa, na inaunga
mkono uimarishwaji wa ulinzi huo wa watu na mali zao, lakini itaendelea kulaani
matumizi yoyote ya nguvu katika kumzuia mwandishi kutekeleza majukumu yake.
Itumike elimu na busara katika kuwaelimisha makundi yote yanayofika katika
maeneo ya mahakama kuhusu uwepo wa hali ya ulinzi wa namna fulani ili kuondoa
mkinzano wowote utakaowanyima fursa wananchi ya kupata habari.
Lakini pia inawataka waandishi wote wanaokwenda kufuatilia na
kuripoti kesi za mahakamani hasa kesi kubwa kufuata utaratibu wa kuomba kibali
cha mahakama, lakini pia kumuona incharge wa polisi ili kujenga mazingira sawia
ya ufanyaji kazi katika makundi yote matatu: mahakama, polisi na waandishi.
Tunamshukuru Kamanda wa Polisi wa mkoa, Boaz ameanza
kulifanyia kazi na ameshakutana na watendaji wake, kwa lengo la kutafuta namna
bora ya waandishi kutekeleza majukumu yao bila kuathiri shughuli za kipolisi
katika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo ya mahakama.
Imetolewa na
…………………………..
Rodrick Makundi
Mwenyekiti, MECKI
KUNRADHI JESHI LA POLISI NA KLABU
Pamoja na kuwepo kwa maazimio hayo mimikama wanahabari waliothirika na matukio hayo tunaiomba jeshi la polisi kufahamu kuwa katika swala la mahakama hata siku moja hatujawahi kuwa na tatizo na Jeshi la polisi isipokuwa Askari mmoja Mwanamke (Jina na Cheo Tunalo) ambaye bila sababu za msingi ametokea kuwachukia waandishi wa Habari.
Tunadhani kuna haja ya Jeshi kuliangalia swala hili kwa kina maana kulichukulia kama swala la kawaida ni hatari kwa usalama wa Waandishi wa Habari.
Tunaheshimu sana Jeshi la polisi na mamlaka zote katika mahakama zetu na ndio maana kwa busara kabisa tumekuwa tukizungumza na Maaskari walioko Mahakamani, tukishirikiana kuhakikisha kwamba sheria za Mahakama zinazingatiwa.
Kitendo cha Askari huyo kutulazimisha kufuta Picha katika Kamera yetu ni kitendo cha kudhalilisha Tasnia ya Habari au huo ndio Uhuru wa Vyombo vya Habari?
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :