USILOLIJUA KUHUSU UGONJWA MPYA UNAOSABABISHA MWANAMKE KUFIKA KILELENI HATA BILA KUFANYA MAPENZI.
Posted in
No comments
Monday, December 30, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Hata hivyo, katika kundi la magonjwa haya, yapo pia machache sana
ambayo ni wazi wengi wetu yanaweza kutuacha vinywa wazi kwa mshangao
pindi tutakapoyasikia au kuyasoma kwa njia kama ambazo nimeshazitaja
hapo awali, na miongoni mwayo ni hili la Persistent Genital Arousal Disorder ambalo hujulikana kwa kifupisho cha PGAD, kitaalamu.
Naam, huu ni miongoni mwa magonjwa ambayo hayajazoeleka masikioni,
machoni wala akilini mwa mamilioni ya sisi, kwani limekuwa halitajwi
mara kwa mara, pengine kutokana na uchache wa wenye kuugua gonjwa hili.
Je, PGAD ni ugonjwa gani hasa?
PGAD, ni ugonjwa wenye kuwahusu zaidi wanawake. Ni hali ambayo humfanya mwanamke kufikia kilele (mshindo), ule ambao kwa kawaida hufikiwa kwa kushiriki tendo la ndoa, lakini katika muktadha huu, humtokea mwanamke bila kushiriki tendo hilo na ukisababishwa na vitu ambavyo havihusiani kabisa na mapenzi.
Ugonjwa huu ambao kiasili ulijulikana kwa jina la kitaalamu la
Persistent Sexual Arousal Syndrome (PSAS), na ambao pia baadhi ya
wataalamu wamekuwa wakiuita Restless Genital Syndrome (ReGS/RGS),
hutokana na hali ya viungo vya uzazi vya mwanamke kuwa katika hali ya
ashki isiyodhibitika kila wakati tena akiwa hayuko kabisa katika
mazingira au kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mara ya kwanza kabisa, taarifa za ugonjwa au hali hii ziliweza
kuandikwa na daktari Sandra Leiblum, mnamo mwaka 2001, na katika siku za
karibuni umeendelea kuvutia hisia za wataalamu zaidi kuufanyia
uchunguzi na kufanya machapisho yenye kuuhusu.
Wengi wa wataalamu wamekuwa wakieleza kuwa ugonjwa huu ni wenye
kuwakumba wanawake zaidi, huku wachunguzi zaidi wakiufananisha na ule wa
"Priapism" ambao huwakumba wanaume zaidi. Ni miongoni mwa magonjwa
ambayo taasisi za kimataifa za tafiti za maradhi, zimeamua kuanza
kuutambua rasmi, miongoni mwazo ikiwa taasisi ya American Psychiatric
Association.
Mbali ya kutokuwa ugonjwa wenye kufahamika, pia kumekuwa na uhaba wa
taarifa za wenye kuumwa ugonjwa wenyewe ambapo wenye kukabiliwa na
tatizo hili wamekuwa wakilichukulia kama gonjwa la kufedhehesha kuweza
kulitamka hadharani, huku kutokuwepo kwa umakini katika jamii zetu juu
ya matatizo ya mifumo ya viungo vya uzazi, ikielezwa kuwa sababu yenye
kuwaacha wenye tatizo hili wakiendelea kuteseka.
Dalili za PGAD:
Hali ya kupandwa na ashki yenye kusababishwa na tatizo hili, huelezwa kuwa ni yenye kuweza kusababisha maumivu ya kimwili na zaidi ya kisaikolojia, huku ikitajwa kuwa ni yenye kuweza kuchukua muda wa siku kadhaa hadi mawiki kadhaa pia. Kwa mwenye kukabiliwa na tatizo hili, hali ya kuweza kufika kileleni huweza kumsaidia kupunguza kiasi maumivu, lakini kinachokwaza sana ni kuwa licha ya hilo, bado ashki huweza kumshika mtu huyo huyo ndani ya muda mfupi sana wa hata chini ya saa moja.
Kurejea kwa hali ya ashki mara nyingi huwa ni kwa ghafla na
kusikotarajiwa, na kuna wakati hali huwa mbaya zaidi ambapo mhusika
hujikuta akiwa anafikia mshindo mara kwa mara kila anaposhikwa na ashki
hizo. Zipo taarifa za wanawake wawili ambao walishajitokeza hadharani,
mmoja akisema huweza kufikia mshindo walau mara 50 kwa siku, na mwingine
aliyetoa ushuhuda wa kuwa huweza kufikia hata mara 200 ndani ya saa 24.
Ingawa haijaweza kufahamika wazi kuwa chanzo cha hali hii ni nini,
lakini miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikitajwa kusababisha kurejea
kwa hali ya ashki hata pale inapotokea kuwa mhusika alishatokewa nayo na
akafikia mshindo, ni pamoja na kuendesha baiskeli, mtetemo wa simu
ikiwa mfukoni na hata kujisaidia haja chooni.
Dalili kuu inayoelezwa kujulikana hadi sasa ni kuwa mhusika hujikuta tu
ameshikwa na hali ya ashki ghafla bila hata kuwa karibu na mpenzi wake
au hata kumuwaza, na kujirudia kwake mara kwa mara katika muda mfupi
mfupi kila baada ya kufikia mshindo baada ya tukio la awali.
Inaelezwa kuwa, miongoni mwa madhara ya ugonjwa huu ni pamoja na
wahusika kujikuta katika hali ya msongo wa mawazo (kutokana na imani
kuwa ni ugonjwa wenye kufedhehesha mbele za watu) huku pia baadhi ya
wahusika wakishindwa kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi kutokana
na kujikuta wakipata maumivu pindi wanapotaka kufanya tendo la ndoa
kiukweli kweli wakiwa na wenza wao.
Katika maelezo yake mmoja wa waliojitokeza kueleza wazi wazi kuumwa na
ugonjwa huu, alibainisha kuwa yeye amekuwa akikumbwa na tatizo la kufika
kileleni (mshindo) kila asikiapo milio ya magari, honi na hata milio ya
vitu vinavyogongana kama pale mtu anapokuwa anagonga kitu kwa kutumia
nyundo.
Yupo mwingine ambaye katika maelezo yake anaeleza kuwa, akisikia tu
muziki unaopigwa kwa sauti ya juu ya besi kubwa basi mambo humharibikia,
hii yote ikionyesha ni jinsi gani tatizo hili lisivyokuwa na sababu
zilizo wazi au "common" miongoni mwa wenye kuwa nalo.
Tiba yake ni nini?
Hadi sasa, haijaweza kujulikana kwa kitaalamu kuwa sababu hasa za tatizo hili ni zipi ingawa wataalamu wa tiba wamekuwa wakieleza kuwa huenda linasababishwa na hitilafu katika mfumo wa ubongo wa mwanadamu. Na hali hii ndio ambayo imekuwa ikiwafanya wataalamu wa tiba kubobea zaidi katika kufanya uchunguzi na utafiti wa tatizo hili kwa minajili ya kulipatia tiba baada ya kujua hasa sababu zake ni zipi.
Kweli inayojulikana hadi sasa kuhusu PGAD:
Licha ya mkanganyiko ambao bado ungali umegubika katika suala zima la ugonjwa huu, taasisi moja imeweza kuripoti kuwa, takriban watu 7000 kote duniani wamekuwa na tatizo hili likiwasumbua kwa muda wa miaka kadhaa sasa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako






0 MAOINI :