MWANDISHI WA BBC ALIYEFARIKI DUNIA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA WAZIKWA KWA KUCHOMWA MOTO
No comments
Thursday, January 30, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa
BBC aliyeaga dunia wiki jana Ann Waithera umechomwa katika eneo la
makaburi ya umma la Lang'ata mjini Nairobi.
Ulikuwa wasia wa Ann aliyekuwa anapenda sana
kutunza mazingira kuwa mwili wake uchomwe na kisha majivu yake yatupwe
kwenye mto na mengine kuwekwa katika eneo ambako kutapandwa mti kama
kumbukumbu kwake.
Ann
aliyekuwa na umri wa miaka 39 alifariki baada ya kuugua Saratani ya
ubongo kwa miaka miwili tangu mwaka 2012.Aliwahi kufanya kazi na
mashirika mawili ya
habari nchini Kenya, Nation na Citizen kama mtangazaji wa televisheni
kabla ya kujiunga na shirika habari la kimataifa la BBC.
Katika BBC, alikuwa anafanya kazi kama ripota wa
redio na televisheni hasa alipokwenda Ethiopia, kama ripota wa kwanza
mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza.Wakuu wa idhaa ya BBC Swahili David Okwemba, Ali
Saleh na mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera wamemtaja Ann kama mchapa
kazi na mfanyakazi aliyependa kujituma na kwamba BBC imepoteza mwandishi
habari mahiri sana Afrika.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :