UMOJA AFRIKA KUZUNGUMZIA MIGOGORO AFRIKA
No comments
Thursday, January 30, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma |
Viongozi wa Afrika wameanza
mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao
kuu itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan
Kusini.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa tume ya
Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni
wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili
kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.
Jamhuri
ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa
tangu waasi kuipindua serikali.Katika taifa jirani ya Sudan Kusini,
makundi
hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano
makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati
ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.
Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara.
Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati na Sudan Kusini.Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.
Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha miaka minne.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :