JESHI LA POLISI LINAMSAKA JAMBAZI SUGU TANZANIA
No comments
Thursday, January 30, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
IGP- Ernest Mangu |
Polisi Nchini Tanzania wanamsaka
mtu mmoja aliyewauwa watu nane kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watatu.Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, siku ya Jumamosi usiku eneo la Kaskazini mwa Mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo, Jambazi hilo lilikuwa likitaka kupewa pesa na simu za mkononi toka kwa waathiriwa.
Kikosi maalum kinachojumuisha maafisa wa polisi
wapatao 160 kimeundwa na mekabidhiwa jukumu la kumsaka jambazi huyo kwa nia ya
kumtia mbaroni.
Mwanahabari wa BBC Nchini Tanzania anasema kuwa
sio kawaida kwa watu wa Mara wanaopakana na Ziwa Victoria kubeba bunduki
katika harakati za kulinda mifugo wao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :