STEVE NYERERE ALIA NA "VICHUPI" BONGO MOVIE
Posted in
No comments
Thursday, January 23, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
RAIS wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, amewafunda wasanii wa kike kuhusu suala la mavazi katika filamu.
Steve alikutana na wasanii hao hivi karibuni jijini Dar es Salaam
ambako aliwasisitiza kujiheshimu katika mavazi pindi wanapocheza filamu.
“Nataka heshima irudi katika filamu, si kila mtu anakuwa anacheza
filamu kwa kuvaa mavazi ya kujidhalilisha ya nusu utupu,” alisema Steve.
Aliongeza kuwa ana mkakati wa kuleta mapinduzi katika Bongo Movie ili kurudisha heshima.
“Nimewaambia haiwezekani mama yuko nyumbani eti kavaa kimini na
blauzi ambayo mwili wote na kifua kikionekana.
Wanawake wa Kitanzania
tunawajua na kwa ushahidi hata wao wanatambua, ila wanaleta ukaidi
usiokuwa na maana tu,” alisema Steve na kuongeza kwamba, kwa kuwa filamu
zetu zinapendwa na zinauzwa mbali, wasanii wa kike wanapaswa kuwa
mabalozi wema ndani na nje ya nchi, kwa kumjengea heshima mwanamke wa
Kitanzania.
Alifafanua kuwa kama mtu yuko katika ‘sini’ ya kucheza na nguo za
aina, hiyo hakuna shida, avae lakini haiwezekani kila sehemu waigizaji
wa kike wawe wamevaa nguo za kujibana na fupi zinazowachoresha.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :