MWANAMKE ATAPELIWA MILIONI 5 HOTELI YA FRESH COACH MOSHI

Posted in
No comments
Thursday, February 20, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi.
Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
Akilia kwa Uchungu
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi
Uchungu wa kutapeliwa hela
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.
Msamaria mwema akimsaidia kupanda ngazi za Hoteli hiyo tayari kwa safari ya kuelekea kituo cha Polisi kutoa Taarifa.
Bi. Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka Polisi kutoa taarifa hizo. (picha zote na Kija Elias wa Kijiwe chetu blog)

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .