MBUNGE MOSHI VIJIJINI ALIA KUCHEZEWA RAFU FACEBOOK
Posted in
Siasa
No comments
Saturday, March 29, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Ripota Wetu, Moshi
Jinamizi la Urais linazidi kutikisa medani za siasa nchini, baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami (CCM) kudai anaandamwa na mtandao wenye malengo ya Urais 2015.

Dk.
Chami amedai kiini ni mbabe mmoja ambaye hakumtaja, mwenye uwezo wa
fedha kukasirishwa naye, baada ya kukataa maagizo yake kwamba amsaidie
swahiba wake anayewania Urais mwaka 2015.
“Niliikataa
kazi hiyo kwa sababu haina maslahi kwa Taifa wala Moshi Vijijini…Mimi
nitamuunga mkono mgombea Urais yeyote atakayechaguliwa na mkutano mkuu
wa CCM,”alisema Dk. Chami.
Dk.
Chami aliongeza kusema,”Haitanishangaza ikithibitishwa kuwa mbabe huyu
ndiye anatoa fedha kuufadhili mtandao huu wa wahalifu, japo hii ni kazi
ya Polisi na ni kazi inayoendelea,”
Mbunge
huyo amedai mtandao huo, ndio ambao umefungua akaunti yenye jina lake
na picha katika mtandao mashuhuri wa kijamii wa Facebook na
kumchonganisha na wapiga kura wake na CCM.
Katika
taarifa yake kwa gazeti hili jana, Dk. Chami amedai akaunti hiyo
inatumika kumchonganisha na chama chake pamoja na viongozi wakuu wa CCM
ili asiteuliwe kugombea ubunge mwaka 2015.
“Kwa
kujifanya wao ni mimi, wanapingana na misimamo yote ya CCM. Kwa mfano,
wanadai kuwa kwenye mchakato unaoendelea wa Bunge la Katiba, mimi
napendelea serikali tatu,”amelalamika.
Akitoa
mfano wa hivi karibuni kabisa, Dk. Chami amedai Jumapili iliyopita,
watu hao walitoa taarifa kuwa ana mashaka CCM itashindwa huko Kalenga
kwa kuwa mara zote kinashinwa chaguzi ndogo.
“Eti
mimi napendelea kura ya siri katika Bunge la Katiba linaloendelea….
Naonyeshwa kuwa mtetezi wa CHADEMA na kutabiri ushindi wa Chadema huko
Kalenga na Chalinze”amelalamika Dk. Chami.
Dk.
Chami amesema akaunti hiyo ya Facebook sio yake na kwamba kama analo
jambo anataka kuzungumza na wapiga kura wake, atawafuata jimboni na si
kuzungumza nao kupitia Facebook.
Pia
amesema tayari amewasiliana na viongozi wa CCM juu ya uwepo wa uhalifu
huo ambao lengo ni kutaka kumuonyesha kuwa yeye ni msaliti ndani ya CCM
jambo ambalo hata halifikirii kulifanya.
Dk.
Chami amekilaumu kitengo kinachoshughulikia makosa ya mitandaoni (Cyber
Crime Unit) kwa kushindwa kuifunga akaunti hiyo na kuwakamata
walioifunga na wanaoendelea kuitumia.
“Tena
akaniambia waliomba msaada TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzania) ili akaunti hii ifungwe, nao TCRA wameshindwa”alilalamika Dk.
Chami.
“Hadi
leo akaunti inatumika naendelea kutengenezewa maadui ndani ya CCM na
kwa viongozi wa juu wa nchi na wahalifu hawa wako huru wakiendelea
kuchekelea maumivu wanayonisababishia”amedai.
Dk.
Chami amesema japo ameshauri na Polisi kwamba naye aingie Facebook na
kuwajibu wahalifu hao, kamwe hatafanya hivyo kwani anaweza kuchochea
taarifa mbaya zaidi kuliko sasa.
“Nimekataa
kwa sababu kama wahalifu wameweza kuniundia akaunti na Dola imeshindwa
kunilinda, nikiunda akaunti yangu wataiingilia na hiyo na wataandika
mabaya kuliko wanayoyaandika”alisema.
Dk.
Chami alisema kama wahalifu hao wataweza kuingilia akaunti yake na
kuandika mabaya zaidi kwenye akaunti yake halali, watasherehekea na
kuhalalisha uovu wao huo.
Soma taarifa yake kamili hapa chini
Naitwa Dr Cyril August Chami,
Mbunge wa Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Kwa miezi
kadhaa sasa kuna mtu au kikundi cha watu ambaye/ambacho kimeunda akaunti
feki kwenye Facebook kwa jina langu na kuitumia akaunti hiyo.
kunichonganisha na Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi mbali mbali nchini Tanzania kwa lengo kuu moja: kunipaka matope na kuichafua taswira yangu mbele ya umma na ndani ya CCM.
Wanachokilenga (na hapa natumia wingi kwa sababu ndivyo nimeelezwa na Cyber Crime Unit of the Police Force Tanzania) ni kupambana nami kupitia mitandao ili tu 2015 nisiteuliwe na CCM kuendelea kugombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini, ateuliwe mwanachama mwingine wanayemtaka wao!

Kwa kujifanya wao ni mimi, wanapingana na misimamo yote ya
CCM. Kwa mfano, wanadai kuwa kwenye mchakato unaoendelea wa Bunge la
Katiba, mimi napendelea serikali tatu. Eti mimi napendelea kura ya siri
katika Bunge la Katiba linaloendelea.
Naonyeshwa kuwa mtetezi wa CHADEMA. Hata katika uchaguzi uliofanyika March 16 Kalenga eti naonyeshwa "kutabiri" ushindi wa CHADEMA na pia eti "nimetabiri" ushindi wa CHADEMA Chalinze!
Naonyeshwa nikijinasibu kuwa eti Chama changu CCM huwa kinashindwa chaguzi ndogo, kwa hiyo na hizi mbili CCM ijiandae kushindwa! Wahalifu hawa wanayatuma maoni haya yote kwa niaba yangu huku wakisahau kabisa kuwa ni hivi majuzi tu tarehe 9 Februari CCM ilivigalagaza vyama vya upinzani kwenye uchaguzi MDOGO wa madiwani kwa kushinda katika kata 23 kati ya kata 27.
Ama kwa makusudi kabisa, ama kwa upungufu wao wenyewe wa kumbukumbu, au kwa ushabiki wao kwa upinzani, wanatabiri kwa niaba yangu kuwa CCM ni dhaifu kwenye chaguzi ndogo, kitu ambacho ni kichekesho kwa sababu takwimu ziko wazi:
CCM imewika uchaguzi mdogo wa madiwani, CCM imewika Kalenga, na kila mtu anayefahamu siasa angalau ya darasa la saba anajua kuwa CCM itawika Chalinze!

Kutokana na uhalifu huu, nimechukua hatua zifuatazo:
Kwanza nimeikana akaunti hiyo ya Facebook. Siyo yangu na
situmii mitandao ya kijamii katika siasa kwa sababu kuu mbili.
Sababu ya kwanza ni kwamba asilimia kubwa ya walioniajiri yaani wapigakura wa Moshi Vijijini hawatumii mitandao ya jamii. Kwa hiyo hata kama ningeandika mafanikio yote ya uongozi wangu kwenye Facebook ni asilimia ndogo sana ya wapiga kura wangu ingenisoma. Ni kweli kuwa Watanzania wanaoishi mijini au kwenye diaspora wangeelewa, lakini mwisho wa yote wengi wao hawatapanda ndege au magari ili tu kwenda Moshi Vijijini kunipigia kura.
Nitoe mfano kuwa mwaka 2005 ilipigwa kura ya maoni kwenye mtandao mmoja wa jamii kuhusu nani angeshinda ubunge Moshi Vijijini. Mgombea wa CHADEMA "alishinda" kwa asilimia 80. Mimi "niliambulia" asilimia 20. Kwenye uchaguzi "halisi" nilipata kura 49,000 na mgombea wa CHADEMA akapata kura 18,000!

Pili, badala ya kuandika kwenye Facebook au mitandao
mingine ya kijamii, nimegundua njia rahisi na yenye uhakika ya
kuwaongoza wananchi walionichagua. Njia hiyo ni kuwafuata huko waliko.
Katika miaka takriban tisa ya ubunge wangu nimewatembelea wapiga kura wangu walio katika vitongoji 322, vijiji 67 na kata 16 kuliko mbunge mwingine yeyote tangu Tanzania iwe huru. Kwa hakika, takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya ziara zangu za miaka tisa inaizidi jumla ya ziara za watangulizi wangu wote kwa miaka 40.

Hii haina maana kuwa sikutani na wapiga kura wangu
wanaoishi nje ya jimbo. La hasha! Bado nakutana nao. Kwa mfano, tarehe 2
Februari mwaka huu nilikutana na wapiga kura wangu wanaotoka Kata ya
Uru Mashariki (Kinyamvuo) waishio Dar es Salaam ukumbi wa Chuo cha Maji.
Baada ya kuwaeleza hali ya kata yao na kuyajibu maswali yao, msemaji aliyesimama kunishukuru, Mheshimiwa DC mstaafu Clemence Orauya, alikiri kuwa katika hadhira ile ya watu karibu 300 hakuweko mtu anayeifahamu jiografia ya kata ile kama mimi, japokuwa mimi si mzaliwa wa kata hiyo. Aliungwa mkono na karibu kila aliyehudhuria.

Kwa ufupi, Facebook haiwezi kumfikia mwananchi aliyeko
kitongoji cha Uhondo au Saningo au Mandaleni au Msarikie ambako kote
hakuna umeme achilia mbali mtandao; mbunge anaweza. Facebook haiwezi
kusimamia ujenzi wa barabara za Kibosho na Uru kwa kiwango cha lami;
mbunge anaweza.
Facebook haiwezi kuikumbusha Serikali ianzishe ujenzi wa barabara ya lami ya Old Moshi kama ilivyoahidiwa; mbunge anaweza. Facebook haiwezi kusimamia sekta ya elimu Moshi Vijijini; mbunge anaweza. Facebook haitatatua tatizo la maji katika Skimu ya Umwagiliaji Lower Moshi; mbunge anatatua kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.

Hatua ya pili niliyochukua ni kuwasiliana na uongozi wa CCM
ngazi za wilaya, mkoa na taifa kuwaeleza juu ya uwepo wa uhalifu huu.
Hivyo, picha inayotengenezwa kuwa mimi ni msaliti ndani ya CCM ni sawa
na kumtupia tope mtu aliyejipaka mafuta! Tope zote zinadondoka bila
kumchafua mlengwa.
Hatua ya tatu ni kutoa taarifa Makao Makuu ya Polisi Dar es
Salaam Kitengo cha Makosa ya Uhalifu kwenye Mitandao (Cyber Crime Unit)
ili wanisaidie kuifunga hiyo akaunti na kuwakamata wahalifu. Kwa
masikitiko makubwa sana wameshindwa yote mawili. Hadi leo akaunti
inatumika; hadi leo naendelea kutengenezewa maadui ndani ya CCM na kwa
viongozi wa juu wa nchi; na hadi leo wahalifu hawa wako huru wakiendelea
kuchekelea maumivu haya wanayonisababishia.
Nina hakika watakaposoma ujumbe huu watakuwa hawana mbavu kwa vicheko huku wakijipongeza kwa kuyafanikisha malengo yao.

Kwa masikitiko makubwa zaidi, kiongozi wa Cyber Crime Unit
ameniambia wameshindwa yote mawili!!!! Wameshindwa kuifunga akaunti
hiyo;
na wameshindwa kuwatambua wahalifu hao, na kwa maana hiyo wameshindwa kuwakamata. Walichofanikiwa hadi sasa ni jambo moja tu, nalo ni kugundua kuwa uhalifu huu unafanywa na kikundi cha watu waliojipanga kiujanja kiasi kwamba wao (Cyber Crime Unit) wamewashindwa. Tena akaniambia waliomba msaada Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority-TCRA) ili akaunti hii ifungwe, nao TCRA wameshindwa!

Nayaandika haya yote kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza ni
ile inayotegemewa na msomaji yeyote, nayo ni ile ya haki yangu binafsi.
Naamini ninayo haki ya kulindwa kutokana na uhalifu huu kama msomaji
yeyote alivyo na haki hiyo. Binafsi natambua wahalifu hawa
wanachokilenga ni kimoja tu: Dr Chami
asiwe tena mbunge wa Moshi Vijijini kuanzia 2015.
Wanajua hadi sasa hakuna mwana CCM mwenye ubavu wa kunishinda katika kura ya maoni mwakani. Hivyo njia pekee ni kunichonganisha na wakuu wangu wa CCM ili nitakaposhinda kura ya maoni, ngazi za juu za CCM ziache kuniteua ateuliwe mtu mwingine. Kwao haijalishi kama mgombea huyu mbadala atakipatia ushindi CCM.
Kwao ni heri upinzani uchukue jimbo lile kuliko Dr Chami awe mbunge. Kwa ufupi, hawa sio wapenzi wa CHADEMA au CCM. Ni wababe wenye fedha wanaoamini wana uwezo wa kumuinua yeyote awe mbunge na kumshusha yeyote asiwe mbunge.
Na kwa sababu walishanieleza nia yao hiyo na nimeyaeleza haya yote kwa Polisi, najisikia huru kuwaeleza wasomaji kiini cha tatizo lenyewe. Kiini ni kwamba mbabe mmoja mwenye fedha amekasirishwa nami kwa sababu nimekataa maagizo yake kuwa nimsaidie swahiba wake anayewania Urais 2015!
Niliikataa kazi hiyo kwa sababu moja tu: Haina maslahi kwa Taifa wala Moshi Vijijini!!!!! Mimi nitamuunga mkono mgombea Urais yeyote atakayechaguliwa kwenye mkutano mkuu wa CCM, siye mgombea ninayelazimishwa nimuunge mkono nje ya mfumo halisi wa CCM na kinyume na dhamira yangu.

Haitanishangaza ikithibitishwa kuwa mbabe huyu ndiye anatoa
fedha kuufadhili mtandao huu wa wahalifu, japo hii ni kazi ya Polisi na
ni kazi inayoendelea. Kama mtandao huu utashinda au utashindwa ni jambo
la "tusubiri tuone".
Ninalothibitisha kwa wasomaji ni kuwa mimi nitaendelea kuwa mwaminifu kwa wapigakura wangu wa Moshi Vijijini na kwa Chama cha Mapinduzi (CCM). Wao wakiamua niendelee kuwawakilisha nitaendelea. Wakinitaka nipumzike nitayaheshimu maamuzi hayo na nitafanya mambo mengine. Ikumbukwe kuwa kabla ya kuwa mbunge sikuwa barabarani. Nilikuwa nafanya kazi na nitaendelea kufanya kazi.

Sababu ya pili iliyonifanya niandike ujumbe huu ni
kuonyesha hofu yangu kwa nchi yetu ya Tanzania kuwa uhalifu unaweza
kufanywa NA VYOMBO HUSIKA VYA DOLA VIKAKIRI KUSHINDWA. The Cyber Crime
Unit of the Police Force and the TCRA have both confirmed their
helplessness on this matter!
Hii ina maana gani?
Ina maana kuwa wakimalizana nami watafanya hivyo kwa yeyote
wanayemchukia na vyombo vya dola vitakiri kuwa haviwawezi. Lakini mbaya
zaidi, wataiingilia sekta ya fedha na kuwaibia wananchi bila huruma na
vyombo vya dola vitakiri kuwa hawawawezi wahalifu hawa!
Nimeshauriwa na Cyber Crime Unit kuwa nami niingie Facebook
kuwajibu wahalifu hawa. Nimekataa kwa sababu kama wahalifu wameweza
kuniundia akaunti na dola imeshindwa kunilinda, nikiunda akaunti yangu
wataiingilia na hiyo na wataandika mabaya kuliko wanayoyaandika kwenye
akaunti waliyounda wao.
Hii ni kwa sababu kwenye akaunti waliyounda wanaogopa kufanya uharibifu mkubwa wakijua kuwa siku si nyingi watagunduliwa. Lakini wakiweza kuiingilia akaunti niliyoisajili mwenyewe watasherehekea kwa sababu wataweza kuandika mabaya zaidi kupitia akaunti yangu halali na kuyahalalisha kabisa haya ambayo wameshaandika.
Hapo hata wale wasomaji wanaoamini kuwa nahujumiwa wataniona msanii na CCM wataniita rasmi msaliti. Lengo la wahalifu litatimia na Cyber Crime Unit wataendelea kuniambia wameshindwa kuwapata "perpetrators" hao.

Wasalaam,
Dr Cyril Chami.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :