ALIBABA AMDUNDA ROY MMBUNDA KWA KO

No comments
Sunday, April 6, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Kikundi cha ngoma kikitoa Burudani kabla ya pambano la Ngumi kuanza kati ya Bondia Alibaba Ramadhan wa Kilimanjaro na Roy Mbunda wa Ruvuma.
Mgeni rasmi katika pambano hilo mkuu wa polisi wa wilaya OCD Deusdedit Kasindo akizungumza kabla ya kuanza kwa pambano la ngumi katika ya bondia Alibba na Roy Mbunda.
Mwakilishi wa kampuni ya Panone ,Gido Marandu akizungumza kabla ya pambano hilo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akizungumza kabla ya pambano hilo.
Mmoja wa mabondia waliopambana katika mapambano ya utangulizi akitokwa mchuzi baada ya kuchezea masumbwi toka kwa Bondia Mwakipesile.
Bondia Mwakipesile(Shoto) akisukuma konde .
Hatimaye bondia Mwakipesile akaibuka mshindi kwa pointi
Likafuata pambano la Bondia Massawe toka kibosho .
Akapambana na Bondia Rasta toka jijini Arusha.
Bondia Rasta akachezea ngumi za kutosha toka kwa Mkibosho.Masawe.
Bondia Rasta akaomba Poooo.akasalimu amri akasema siendelei na pambano taumia.
Bondia Masawe toka Kibosho akapewa Ushindi kwa kumtwanga  KO Bondia Rasta.
Bondia Rasta akifurahia ushindi.
Likafuatia pambano kali tena na hapa ni kati ya Fredy George kutoka Himo mwenye Bukta ya njano na Pascaly Bruno wa Moshi.
Ngumi zikapigwa kwa raund zote nne.
Mabondia wote wakiwa hoi kama anavyoonekana Fredy George akivuliwa Groves.
Bondia Pascaly Bruno akatangazwa mshindi .
Baadae sasa likafuata pambano lililokuwa likisubiriwa na wengi ni la kuwania mkanda wa taifa kati ya Bondia Alibaba Ramadhan na Roy Mbunda.
Bondia Alibaba Ramadhan akiingia ukumbini akiwa anasindikizwa na wapambe wake.
Bondia Alibaba akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa pambano.
Pambano likaanza ndani ya round ya pili tu Bondia Alibaba anasukuma konde kwa bondia Roy Mbunda lililompeleka chini.
Baadae Roy Mbunda akaamka akigugumia maumivu ya mguu akidai msuli wa paja umebana.
Mwamuzi wa pambano hilo Said Chaku akalazimika kutaka kufahamu endapo Mbunda ataendelea ama la.
Mwamuzi Chaku akalazimika kukatisha pambano kutokana na Bondia Mbunda kuda hatoweza endelea na pambano.
Roy Mbunda akisikilizia maumivu.
Maumivu yakamzidi Roy Mbunda na kuanza kuangua kilio.
Mashabiki nao walilipuka kwa kelele.
Hatimaye madaktari ikawalazimu kuingia ulingoni kutoa huduma ya kwanza kwa Roy Mbunda.
Akanyooshwa viungo.
Bondia Alibaba Ramadhan akatangazwa bingwa wa taifa .
Kisha akavalishwa mkanada wake wa Ubingwa akapata picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi pamoja na wadhamini.

Ngumi iliyompelleka chini Roy Mbunda ilisababisha pia uharibifu wa kamba za Ulingo na hapa ni baada ya bondia Mbunda kudondokea .

Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Kilimanjaro Elikunda Kipoko pamoja na wadhamini wakifurahia ushindi wa Alibaba.
Akapongezwa Roy Mbunda.
Akapongezwa Alibaba kwa ushindi na sifa aliyoupatia mkoa wa Kilimanjaro.
Bondia Abdallah Mwakipesile wa Moshi manispaa (Glove Nyekundu), akipambana na Emanuel Massawe wa Kibosho, katika pambano la awali uzito wa Kilo 60, kabla ya mpambano wa Ubingwa wa Taifa kati ya Alibaba Ramadhani na Roy Mmbunda, uliopigwa jana usiku katika ukumbi wa YMCA.
Bondia Paschal Bruno (nyeupe), akikipiga na Fredi George (njano) katika moja ya mapambano ya utangulizi ambao ulishuhudia Bruno ambaye ni kocha wa Alibaba akiibuka mshindi wa pambano hilo, kilo 70.
Promoter Andrew George kutoka Green Hills Promotion akionesha mkanda uliowania jana na Mabndia Alibaba Ramadhani na Roy Mmbunda, mkanda wa WBO ubingwa wa Tanzania, kilo 76.
Mwenyekiti wa Chama cha Boxing mkoani wa Kilimanjaro (KBA) Eliakunda George Kipoko akizungumza neno kabla ya kuanza kwa mapambano
Mgeni Rasmi, mkuu wa Polisi Moshi, OCD Kasindo
Mdhamini wa pambano la uzito wa kati (supper middle) kati ya Alibaba na Roy mmbunda, mkurugenzi wa Ibra line, Ibra Shayo
Bondia, Alibaba Ramadhani wa Kilimanjaro (aliyevaa nyekundu),  akipambana dhidi ya Bondia Roy Mmbunda wa Ruvuma, katika mpambano wa  uzito wa kati, ubingwa wa taifa, uliopigwa juzi katika ukumbi wa YMCA,wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Alibaba alishinda mpambano huo  kwa KO.
Katika picha ya Pamoja baada ya Alibaba kutawazwa Bingwa wa Tanzania jana, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa KBA, George Kipoko, mkurugenzi wa Ibraline, Ibra Shayo, Alibaba Ramadhani (mwenye mkanda), Mgeni Rasmi OCD Kasindo na Meneja wa Panone, Gido Marando.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .