TPA YATOA MSAADA WA MADAWATI 110 SHULE YA MSINGI MAHUMBIKA MKAONI LINDI
Posted in
Biashara
No comments
Sunday, April 6, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela
(kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni
20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla
ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika
kilichopo Lindi vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom
Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya
shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa
shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dkt. Hemid Nassoro akizungumza na wakazi wa kijiji
cha Mahumbika kabla ya kupokea msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi
milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za
mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela
akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani
ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila hivi
karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika
wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye
thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi
vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakiimba
wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye
thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi
vijijini.
Wasanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika,
Lindi wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110
yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika
kilichopo Lindi vijijini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :