KUELEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO MJINI ZANZIBAR

Posted in
No comments
Saturday, April 19, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Muungano katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Muungano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, akizungumza machache wakati akimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua Kongamano la Muungano leo.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua Kongamano la Muungano kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, leo Aprili 19, 2014.
Viongozi waliohudhuria Kongamano hilo, wakiwa meza kuu. Wa pili (kulia) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kushoto) Makamu wa pili wa Rais wa Zanznibar, Balozi Seif Iddi, (wa pili kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud. Picha na OMR

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .