MATUKIO MBALIMBALI KATIKA AJALI YA TRENI ILIYOCHUKULIWA NA MAFURIKO
No comments
Wednesday, April 2, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa
mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa
kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo
watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa
katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu
ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali
iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea
saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na
kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari
na mafuta.
Njia
ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya
Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali
nchini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji
baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na
maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo,
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi.
Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa
na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani Mpwampwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa
Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe
Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin
Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya
mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha watu wawili
na wengine saba kujeruhiwa.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :