USAJILI MBIO ZA SOKOINE MINI MARATHON 2014 WAANZA RASMI

Posted in
No comments
Wednesday, April 2, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Namba zimeanza kutolewa kwa washiriki wa mbio za Sokoine Mini Marathon Km 21 na Km 2 ambazo zitatimua vumbi Aprili 12, 2014 Monduli mkoani Arusha, rais Jakaya Kikwete ndiye atakayepuliza kipenga cha kuanza mbio hizo.

Ada ya namba ni Tsh: 2,000 tu, namba zinapatikana Arusha pale Uwanja wa kumbukumbu ya SHEIKH AMRI ABED KARUME na Monduli pia.

Kwa washiriki wote nje ya mkoa wa Arusha wasiliana na VICTOR MACHOTA kwa 0787415864 ambaye atapokea usajili kwa njia ya simu na namba yako utajulishwa kwa SMS na itahifadhiwa hadi utakapoichukua. Mwisho wa kuchukua namba yako ni Ijumaa April 11, 2014 Arusha mjini.

Kwa wale watakaosajili kwa njia ya simu tunaomba mtume hela kwa AIRTEL MANEY kwa namba ya Victor Machota, unaombwa uongezee gharama kidogo ya kutoa pesa mtandaoni.

Kwa wale watakaosajili namba papo kwa papo wawasiliane na PHAUSTIN BAHA 0753860668 kwa maelezo zaidi na kwa wale wa Monduli wawasiliane na ROBERT MOLEL kwa 0753739128.

Kwa ratiba kamili hapo baadae pitia blogu zifuatazo; 
 
WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI NA RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA.

             wazalendo25.blogspot.com
          victormachota.blogspot.com
         Kijiwechetu.blogspot.com
         gidabuday.blogspot.com

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .