ASKARI CHUO CHA POLISI MOSHI WAFANYA UTALII WA NDANI MLIMA KILIMANJARO
Posted in
Utalii
No comments
Monday, May 19, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
| Ofa ya utalii wa ndani katika mlima Kilimanjaro ilijumuisha watu wa Kila Rika,hapa mmoja wa watalii wa ndani akiwa na mtoto wake mgongoni. |
| Kiasi safari ilikuwa ngumu kwa baadhi ya watalii wa ndani |
| Kila hatua zilizo pigwa wataalii wa ndani walipenda kuchuku Taswiras. |
| Na safari iliendelea hapa ikiongozwa na mkufunzi mkuu wa chuo cha polisi Moshi ,SSP,Grayfton Mushi. |
| Baadhi ya watalii walionekana kuchoka lakini kila walipoulizwa walidai wameweka pozi la picha. |
| Safari ya baba na mwana iliendelea ,Mgongoni ni Mtoto Matinde Chacha akiwa na baba yake John Chacha. |
| Hatimaye watalii wakafika Shira Hut,wengine wakiwa wametupia mavazi ya Suti. |
| Afande akiwa hoi baada ya safari ya saa moja ya kufika Shira Hut. |
| Waliofika wakafurahia madhari nzuri na kupata Taswira ya pamoja. |
| Safari ya kuelekea katika mapango ya Shira(Shira Caves)ikaanza tena kutoka Shira hut. |
| Mkuu wa mafunzo katika chuo cha taaluma ya Polisi ,Grayfton Mushi akipozi huku mwenzake Moses Ruvinga ambaye pia ni afisa katika chuo hicho akichukua taswira. |
| Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa ndani ya moja ya Mapango ya Shira yaliyoko katika mlima Kilimanjaro. |
| Watalii wa ndani wakiwa katika eneo hilo la Mapango. |
| Watalii wa ndani wakatembelea eneo la Shira Camp kujionea watalii wanavyo lala wakati wakifanya safari ya kuelekea katika kilele cha Kibo . |
| Hapo wakakutana na Wabebaji wa mizigo ya watalii maarufu kama Wagumu na kupata nyinmbo mbalimbali. |
| Waliopanda na vazi la Suti wakaonesha vipaji vyao vya kusakata Kiduku, |
| Wengine walipata fursa ya kupiga picha na watalii waliokuwepo katika kituo hicho. |
| Kutokana na kuchoka wengine waliamua kupumzika katika machela maalum ya kushushia watu waliozidiwa mlimani. |
| Baadae safari ya kurudi toka mlimani ikaanza. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :