WASHINDI WA MAISHA PLUS NA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 WAPATIKANA NA KUONDOKA NA MILIONI 50
Posted in
Utalii
No comments
Monday, May 19, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Bahati Muriga mshindi
wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tzshs.
Milioni 25 aliyoshinda kwa ajili ya vifaa vya kilimo. Kutoka kulia ni Babu wa
kijiji, Epheta Msiga wa DMB na Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam.
Mshiriki Boniphace Meng'anyi Nyakena akipokea
mfano wa hundi ya Tzshs. Milioni 25 alizoshinda katika msimu huu. Kutoka kulia
ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Jane Foster, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kuyandabila, Babu wa kijiji, mwakilishi
kutoka Datavision International pamoja na Epheta Msiga ambaye ni afisa mradi wa
Maisha Plus kutoka kampuni ya DMB.
Mshindi wa Maisha Plus Boniphace Meng'anyi Nyakenaakiwa na Bahati Muriga mshindi
wa Mama Shujaa wa Chakula 2014
Hizi ni tuzo mbalimbali za Mama shujaa wa Chakula ambazo zilitolewa kwa washiriki wote
Mkurugenzi
Mtendaji wa DMB ambao pia ni waandaaji wa shindano la Maisha Plus
Masoud Ally (Kipanya) akiwa anatoa Miongozo mbalimbali wakati wa Sherehe
hizo za kumpata mshindi wa Maisha Plus Na mama Shujaa wa Chakula 2014
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa Hotuba yake wakati wa
Fainali za kumpata mshindi wa Maisha Plus na Mama shujaa wa Chakula 2014
Mgeni Rasmi katika Fainali za kumpata Mshindi wa Mama
Shujaa wa Chakula na Maisha Plus 2014 Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kuyandabila
akitoa hotuba yake
Mwakilishi
kutoka EKEMA Hilda Mashauri wakitangaza zawadi yao ya Tsh 500,000
wakati wa Fainali za Shindano la Kumpata Mshindi wa Maisha Plus na Mama
Shujaa wa Chakula.
Mwakilishi
kutoka Forum CC Ibrahim Mhazi akitangaza zawadi yao ya Tsh 1,000,000
wakati wa Fainali za kumpata Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus 2014
jana katika kijiji cha Maisha Plus
Mwakilishi
kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitengo cha Jinsia Halima Komolanya
akitangaza zawadi yao ya Tsh 500,000 wakati wa Fainali za kumpata
Mshindi wa Maisha Plus na Mama shujaa wa Chakula
Mwakilishi
kutoka Data vision International wakitangaza
zawadi yao ya Laptop moja kwa Mshindi wa pili wa Maisha Plus
Mwakilishi
wa Katibu Wizara ya Maendeleo, Jinsia na watoto Daniel Wambura
akizungumza jambo wakati wa Fainal za Maisha kati wa Fainali za kumpata
Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus 2014 jana katika kijiji cha Maisha
Plus.
Mwakilishi
kutoka Adon Lodge Mrs. Watengakiwaya akitangaza zawadi yao ya Shamba
lenye ukubwa wa Heka mbili kwa ajili ya kuendeleza Kilimo.
Mshindi wa Maisha Plus msimu uliopita Belenick Kimiro akitoa salam za shukurani na kuvua rasmi nafasi yake.
Khadija
Mwanamboka Balozi wa Mama shujaa wa chakula kutoka Oxfam akitoa salam
zake na kuhimiza kilimo kwa wakulima wadogo wadogo hasa wanawake kwa
kuwa inalipa
Washiriki wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula wakiwa wanafuatilia kwa Makini Fainali hizo
ambapo kati ya hawa kulikuwa na washindi wawili
Walio kaa Mstari wa Mbele ni washiriki wa Maisha Plus ambao walitolewa wakati wa hatua za mwanzoni
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :