KINANA AITAKA SERIKALI KUWAPELEKA MAHAKAMANI VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WALIOTAFUNA FEDHA ZA MALIPO YA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA
No comments
Sunday, May 18, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Fulana
iliyovaliwa na Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Athuman Kapuya
ikiwa na maandishi ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana
wilayani Kaliua, Tabora leo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
mjini Kaliua na kuitaka serikali kuwacvhukulia hatua za kisheria watu
wote walishiriki kuwaibia fedha wakulima wa tumbaku mkoani Tabora.Kinana
yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku 11 ya kuimarisha uhai wa chama,
kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuta Ilani ya CCM,
kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero
za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO
BLOG
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa
hadhara mjini Kaliua leo, ambapo alisema kuwa viongozi wa Ukawa kwa
tabia yao ya uchonganishi na fitina zao kwa wananchi ni kufilisika
kisiasa.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa
CCM mjini Kaliua leo. Aliema kuwa ili kupunguza dhuluma kwa wakulima wa
tumbaku, wakulima kuanzia sasa wameruhusiwa kuuza zao hilo kwa watu
binafsi na vyama vya Ushirika mkoani humo.
Wananchi
wakishangilia kwa kumuita Jembe Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa
alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kaliua.
Mbunge
wa Jimbo la Urambo Magharibi, Athuman Kapuya akihutubia katika mkutano
wa hadhara na kuelezea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata
Ilani ya CCM.
Kinana
akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa pamoja na
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa mkutano wa hadhara
mjini Kaliua.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :