MH. MOHAMMED DEWJI AKIWA KATIKA ZIARA YA KUKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO YA JIMBO LAKE
Posted in
Siasa
No comments
Sunday, May 25, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
MO akisalimiana na wazee wa kijiji cha Uhamaka kabla ya kuanza kuzungumza na wananchi.
MO akisalimiana na mmoja wa watoto waliofika kwenye mkutano wake Uhamaka.
Mbunge MO akilakiwa na mmoja wa bibi kizee aliyefika kwenye mkutano wake , Karibu mjukuu wangu hapa Uhamaka.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akiweka saini kwenye
kitabu cha ofisi ya kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakati akiwa
kwenye ziara ya kiazi ya siku moja kukagua shughuli mbalimbali za
maendeleo katika jimbo hilo, kulia ni diwani wa kata hiyo na Shaban
Kiranga. Kushoto ni mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hassan Mazala.
Diwani
wa Kata ya Uhamaka CCM, Kiranga akimkaribisha Mbunge MO, Katani kwake
kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili sekondari ya Kata hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Uhamaka akisoma taarifa ya ujenzi huo.
Mbunge Dewji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uhamaka wakati wa mkutano wake wa kutembelea jimbo hilo.
Sehemu ya umati wa Kinamama na watoto wa kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakimsikiliza Mbunge wao.
Kikundi cha Ngoma na Kwaya ya kijiji cha Uhamaka wakiimba wimbo wa kumkaribisha Mbunge wao Mohammmed Dewji (MO).
Mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akizungumza kwenye mkutano huo.
Vijana nao walihudhuria mkutano wa Mbunge wao MO katika kijiji cha Uhamaka.
: MO akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ya Uhamaka.
Sheikh wa msikiti wa kijiji cha Ititi akimkaribisha MO.
Sehemu
ya Msikiti wa kijiji cha Ititi ambapo MO aliguswa na kuwachangia mifuko
30 ya Saruji na Mabati 30 kwa ajili ya kuedeleza ujenzi wao.
MO akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu.
Viongozi wa kijiji cha Uhamaka wakiwa ofisini kwao na Mbunge MO .
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ititi, Jumanne Ivanga akisoma taarifa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ititi kwa Mbunge MO.
MO
akihutubia wananchi wa kijiji cha Ititi, pia aliahidi kutoa mifuko 200
ya saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.
“
Kwa hiyo mimi kama Mbunge wenu nitatoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili
ya kukamilisha ujenzi huu sawa jamani.” Alisisitiza MO huku
akishangiliwa na wananchi hao.
Kinamama
wa kijiji cha Uhamaka wakimshangilia Mbunge wa jimbo la Singida mjini
Mohammed Dewji (MO) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua
ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho jana.
Sehemu ya viongozi wa dini na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ititi wakimsikiliza mbunge wao.
Jamani
mmeona utekelezaji wa ilani ya CCM..??? Ni maneno ya MNEC Manispaa ya
Singida, Hassan Mazala akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ititi.
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Mh. Mohammed Dewji akimsikiliza MNEC Hassan Mazala.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ititi Jumanne Ivanga akimwonyesha Mbunge Mh. Mohammed Dewji sehemu ambapo Zahanati hiyo itajengwa.
Muonekano wa sehemu ya Zahanati ya Kijiji cha Ititi itakapojengwa.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akisalimiana na viongozi
wa kijiji cha Unyianga mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya
kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara
jimbo kwake.
MO akicheza na baadhi ya wanakikundi wa uhamasishaji kwenye hafla hiyo.
MO
akisikiliza mashairi kutoka kwa kijana Masoud Mkari mara baada ya
kuwasili kwenye hafla fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya
Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara jimbo kwake.
Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Unyianga, Ramadhani Mpondo akisoma taarifa fupi
ya mradi wa ujenzi wa Sekondari ya kijiji hicho mbele ya Mbunge wa Jimbo
la Singida Mjini.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akizungumza na wapiga
kura wake kuhusu mchango wake katika ujenzi wa shule hiyo inayojengwa
kwa nguvu za wanakijiji pamoja na mfuko wa jimbo la Singida Mjini ambapo
ameahidi mifuko 100 ya Saruji pamoja na Mabati 100.
Ujenzi
wa mradi wa Sekondari ya Kijiji cha Unyianga ulibuniwa na Halmashauri
ya kijiji na kuafikiwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa kijiji baada
ya kubaini changamoto nyingi zinazohusu wanafunzi wanaoendelea na masomo
sekondari ya kata ya Mwankoko ikiwa ni umbali uliopo kati ya Unyianga
na Mwankoko takribani Kilometa 18 kwenda na kurudi, hali inayowalazimu
wanafunzi kutembea umbali mrefu na hivyo kuchoka na kushindwa kufanya
vizuri kwenye masomo.
Baadhi ya wanakijiji wa Unyianga wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :