HIVI NDIVYO BEN PAUL NA IZO BUSINESS WALIVYOPAMBA UZINDUZI WA KAMPENI YA SHUGA REDIO MKOANI IRINGA
Posted in
Matukio
No comments
Tuesday, July 29, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba akitoka kukagua jukwaa lenye hadhi ya kimataifa la Ebony FM kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viunga vya Samora mkoani Iringa.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga wakiwasili kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio inayowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 iliyozinduliwa rasmi jana mkoani humo.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari wakiwemo Shule ya wasichana Iringa wakiendelea kumiminika kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
Stella Shubi kutoka Clouds Media (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika kwenye viwanja Samora mjini Iringa.
MC wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio B 12 kutoka Clouds FM Redio ambao ndio waratibu wa uzinduzi wa kampeni hiyo akiwa na mtoto aliyeashangaza umati wa vijana waliofurika kwenye uzinduzi huo baada ya kujibu swali ambalo hawakutegemea angelijibu kutokana na umri wake.
Meza Kuu, Kutoka kulia ni Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu pamoja na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu.
Baadhi ya Mameneja wa Redio 10 za Jamii zitakazokuwa zikirusha vipindi vya SHUGA Redio vitakavyoanza kurushwa rasmi tarehe 2 Agosti mwaka huu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
Kikundi cha Wazalendo a.k.a Makhirikhiri wa Bongo kutoka Mtwivila Iringa wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
Mohamed Omari kwa jina la usanii Sam wa Wazalendo Group kutoka mjini Iringa akito burudani za nyimbo za Makhirikhiri kwa staili ya aina yake huku akiwa na Nyoka mdomo kwenye sherehe za uzinduzi huo.
Mwanafunzi Calist Hermet wa kidato cha Sita kutoka shule ya Sekondari Tosamaganga akiimba wimbo wenye kuhamasisha matumizi ya Kondomu na upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa vijana huku akipewa sapoti na baadhi ya wanafunzi wenzake katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Kutoka kushoto B Dozen a.k.a B12, Shadee pamoja na Stella Shubi wakiwakilisha Clouds FM Redio ikiwa ni miongoni mwa Redio zitakazokuwa zikirusha vipindi vya kampeni ya SHUGA Redio kupitia kipindi cha Bongo Fleva kinachopendwa kusikilizwa na vijana wengi katika Redio hiyo.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye uzinduzi huo.
Afisa Programu kutoka UNESCO, Courtney Ivins (kushoto) na Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu wakiwa kwenye jukwaa kuu ndani ya viwanja vya Samora mjini Iringa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhiria uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
B Dozen a.k.a B 12 akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga.
Mwanadada Shadee kutoka CLOUDS Media akipata picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi Calist Hermet wa shule ya Sekondari Tosamaganga.
Kwenye moja na mbili alihusika DJ Zero kutoka CLOUDS FM Redio.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi na mashirika mbalimbali walijumuika kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Baadhi ya watoto wa mjini Iringa waliokusanyika uwanjani hapo kushushudia uzinduzi huo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari mkoani Iringa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akizindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio ambapo amewaasa Vijana kuzingatia matumizi sahihi ya Kondomu na upimaji wa VVU ili kuzitambua afya zao mapema na kuepukana na maambukizi mapya ya VVU.
Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amesema Lengo kuu la kampeni ni kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana wa umri wa kubalehe kupitia vyombo vya habari na kuwafikia kwa ujumbe mahususi kuhusu upimaji wa hiari na ushauri nasaha na ngono salama. Kampeni inakusudiwa kuchochea vijana walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi waweze kutafuta na kuziendea huduma zilizopo.
Bi. Jenkins aliongeza kuwa kutakuwa na mfululizo wa vipindi 12 vya kuigiza wenye muda wa dakika nane umeelezea maisha ya vijana wanne (Sofia, Fally, Amina na Kavis) kuwakilisha vijana wa umri wa miaka 15 – 24. Simulizi iliyopo inahusu ndoto, chaguzi, marafiki, mapambano ya changamoto za kimaisha katika Dunia, ambayo UKIMWI ni tishio kubwa.Simulizi hizi kwa ujumla wake zinajikita kwenye somo la mbinu za upimaji wa VVU na ushauri nasaha, matumizi ya kondomu katika mahusiano ya muda mrefu , Kinga, unyanyasaji wa kijinsia na kingono, unywaji pombe na athari za kuwa na wapenzi wengi zinazopelekea kupata maambukizi ya UKIMWI.
Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akimpongeza Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins (kulia) kwa risala nzuri wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu.
Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Iringa, Bw. Owen Wimbo miongoni mwa wadhamini wa kampeni hiyo akizungumza machache na wakazi wa Iringa, Vijana na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu, akizungumza na vijana waliohudhuria uzinduzi huo ambapo aliwaasa kutouza mechi kusubiri muda muafaka na kuzingatia zaidi masomo sanjari na kuepuka kufanya ngono zembe.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu akisikiliza majibu kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Iirnga waliopata nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi akiwa ameungana na wasanii wa Bongo Flava pamoja na meza kuu kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio.
Sasa imezinduliwa rasmi.....!
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari mkoani Iringa wakitumia mbio kutoka kwenye majukwaa yao kusogea uwanja kushuhudia burudani za wasanii wa Bongo Flava Izo Business na Ben Paul waliopamba uzinduzi wa mradi huo jana mkoani Iringa.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Ben Paul akitoa burudani ya aina yake iliyoambatana na ujumbe mahususi wa kuhamasisha vijana kupima afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio ulioanyika jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
Umati wa vijana na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Iringa wakishuhudia burudani za wasanii maarufu wa Bongo Flava waliosinfdikiza uzinduzi huo.
Pichani juu na chini ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini anayejulikana kama Izo Business akitoa burudani kwa Vijana na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
George Magesa kutoka UNICEF (katikati) akipata ukodak na Msanii wa Bongo Fleva nchini Ben Paul pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM Redio B Dozen a.k.a B 12.
Baadhi ya wanafunzi wa Kituo cha Upendo mjini Iringa wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye chumba maalum kwa ajili kupima Virusi vya Ukimwi bure wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Radio uliofanyika kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
Mtaalamu kutoka AMREF akichukua vipimo vya damu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa kituo cha Upendo mjini Iringa aliyejitolea kupima kwa hiari Virusi vya Ukimwi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) sambamba na Redio Jamii 10 nchini Tanzania wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
Vijana wa kiume nao walihamasika kupima afya zao bure bila malipo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :