COASTAL UNION KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE KATIKA COASTAL UNION DAY AMBAYO NI LEO

Posted in
No comments
Sunday, September 7, 2014 By danielmjema.blogspot.com


NA MWANDISHI WETU, TANGA.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kuwatambulisha wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotazamiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.



Utambulisho huo utafanyika leo,  “Coastal Union day” ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7 mwaka huu ambao kufanyika mchezo wa mpira wa miguu ambapo msimu huu Coastal Union itacheza na
Polisi Morogoro kwenye uwanja CCM Mkwakwani.

Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa.

Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.

Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu, Assenga amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

0714543839.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .