MAKUNDI MATANO YAINGIA FAINALI YA DANCE 100% CHINI YA VODACOM

Posted in
No comments
Monday, September 15, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la”Wakali sisi” Buguruni jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akikausha maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wingi wakati shindano la nusu fainali ya Dance 100% na kusababisha shindano hilo kusimama mara kwa mara,Makundi 5 kati ya 10 yaliingia fainali itakayofanyika mwezi ujayo.Shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
Kundi la ”Mazabe Powder ” la Tegeta jijini Dar es Salaam,wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano la dance 100% hapo jana lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Dance 100% wa Kundi la “Quality Boys” la Kinondoni jijini Dar es Salaam,akiwaongoza wenzake wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano la dance 100% hapo jana lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
Wapenzi wa shindano la Dance 100% wakisubiria kwa shindano hilo kuendelea mara baada ya kusimama kwa muda kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wingi wakati shindano la nusu fainali na kusababisha shindano hilo kusimama mara kwa mara,Makundi 5 kati ya 10 yaliingia fainali itakayofanyika mwezi ujayo.Shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.

SAFARI ya shindano la Dance 100% imefikia patamu ambapo hapo jana makundi matano kati ya makundi kumi yaliyochuana vikali katika nusu fainali ya shindano hilo kwenye uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania limeleta mapinduzi makubwa katika tasnia hii na kuweza kuwavutia vijana wengi kushiriki.

Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambayo yamefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha fainali ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,The W.T,Wakali sisi na The winners Crew.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .