SKYLIGHT BAND YATIKISA JIJI LA DAR NYAMA CHOMA FESTIVAL
Posted in
Burudani
No comments
Monday, September 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Sam Mapenzi, Joniko Flower na Hashim Donode wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika miwshoni mwa juma katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mashabiki wakiwa wameshona kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Nyama Choma Festival huku Skylight Band wakitoa burudani ya aina yake.
Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani sambamba na Digna Mbepera kwa mashabiki wa muziki wa Live Band kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM.
Pale Aneth Kushaba AK47 (hayupo pichani) anapogusa mashabiki na uimbaji wake.
Ni hisia tu hakuna kingine....Skylight Band ni balaa.!
Aneth Kushaba AK47 akishambulia jukwaa kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mmoja wa mashabiki akiwa ameshika kiuno kuhamaki kwa kile anachokiona jukwaani kutoka kwa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Aneth Kushaba AK47 akiwapa vionjo vya aina yake mashabiki wa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Digna Mbepera wa Skylight Band akifanya yake jukwaani kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam-UDSM mwishoni mwa juma.
Sam Mapenzi akiporomosha mistari kwa mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Ni burudani mwanzo mwisho.
Sony Masamba akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Mpiga solo wa Skylight Band Allen Kiso Mzuzu akionyesha mbwembwe zake mbele ya camera yetu.
Wapiga vyombo wa Skylight Band wakiwajibika kuhakikisha mashabiki wanapata kitu roho inapenda.
Kwa picha zaidi ingia hapa
Habari Zingine
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :