TAMASHA LA 'HANDENI KWETU LAPANIA KUVUNJA REKODI YA 2013
No comments
Monday, September 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mbwana alisema kuwa hiyo ni kutokana na kutamani kushirikisha wasanii wengi kutoka Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Alisema kwamba mwaka jana wasanii zaidi ya 200 walionyesha uwezo wao kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wilayani Handeni na jijini Dar es Salaam.
“Mwaka jana vikundi zaidi ya 10 vyenye wasanii wasiopungua 15 walipata nafasi ya kupanda jukwaani kuonyesha vipaji vyao, ukiacha wasanii wanaotoka kwenye Kambi ya jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Mgambo waliozidi 80.
“Wakati tunajivunia mafanikio haya, tunaamini msimu huu utakuwa mzuri zaidi tukiamini kuwa tutavunja rekodi ya mwaka jana, ambapo tulishuhudia burudani mbalimbali, ikiwamo hadithi zilizohusu watu wa Handeni, bila kusahau vyakula vya asili pamoja na michezo waliyokuwa wakicheza wazee wetu enzi hizo,” alisema Mbwana.
Kwa mujibu wa Mbwana, mipango ya kuboresha tamasha hilo imepamba moto ambapo kwa sasa utafiti wa ubora wa vikundi nje ya wilaya ya Handeni inafanywa ili kuhakikisha kuwa wasanii watakaopanda jukwaani wanakuwa na uwezo wa juu na kufanikisha kwa dhati kukuza sekta ya utamaduni pamoja na uchumi wa Tanzania.
Habari Zingine
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- Tamasha la Handeni Kwetu lasogezwa mbele, sasa kufanyika Desemba 20
- Machenja ajifua kutoa burudani Tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014
- Tamasha la Handeni Kwetu lawapigia magoti wadhamini
- KWEINGOMA WAAHIDI UHONDO WA NGOMA YA SELO TAMASHA LA HANDENI KWETU 2014
- TAMASHA LA 'HANDENI KWETU LAPANIA KUVUNJA REKODI YA 2013
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :