MBATIA ACHANGIA MILIONI 20 UJENZI WA BWENI,SEKONDARI YA PAKULA JIMBO LA VUNJO.

Posted in
No comments
Tuesday, October 21, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa Mh James Mbatia akiongozana na makamu mwenyekiti wa shule ya sekondari Pakula Julius Furaha(Suti ya Blue) baada ya kupokelewa kwa ajili ya mahafali na harambee ya ujenzi wa Bweni.
Mbunge wa Kuteuliwa ,James Mbatia(NCCR-Mageuzi) akizungumza na viongozi wa shule ya sekondari Pakula iliyopo  kilua Vunjo wilaya ya Moshi vijijini.
Mbunge Mbatia akitoka katika Bweni la Shule ya sekondari Pakula baada ya kutembelea na kutizama hali halisi ya Bweni hilo ambalo Baba yake mzazi,Mwalimu Francis Wiliam Mbatia alishiriki kulijenga.
Mkuu wa shule ya sekondari Pakula akitambulisha wageni wakati wa mahafali ya wanafunzi w kidato cha nne yaliyoenda sanjari na harambee ya ujenzi wa Bweni.
Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Pakula ambao wanataraji kufanya mitihani yao ya mwisho siku chache zijazo.
Baadhi ya wageni kutoka Sweden wakifuatilia shereh hiyo ya mahafali.
Wahitimu wakitoa burudani ya wimbo maalumu wa kuagana wakati wa mahali hayo.
Wanafunzi wa kidato cha tatu wakitoa buruduni kwa kuonesha umahiri wa kucheza muziki .
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Pakula,Paroko Julius Furaha akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya sekondari Pakula Lolenzo John akimkabidhi Mh,Mbatia zawadi ya Mbuzi dume wakati wa mahali ya wanafunzi wa kidadto cha nne katika shule hiyo.
Mh,Mbatia akiwa amembeba mtoto aliyeenda moja kwa moja hadi meza kuu kwa lengo la kumsalimia,
Mh Mbatia akitoa vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kufanya mitihani yao hivi karibuni.
Mh Mbatia akitoa hotuba wakati wa sherhe za mahali katika shule ya sekondari Pakula ,shereh iliyoenda sanjari na harambee ya kuchangia ujenzi wa Bweni.
Mh Mbatia akionesha mkanganyiko uliopo kwenye vyeti vilivyotolewa kwa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne ambapo cheti kimoja kinaonesha kinatolewa na Wizara ya elimu na Mafunzo huku kingine kikitolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Badhi ya wageni waalikwa kutoka mkoani Arusha wakifuatilia hotuba ya Mh Mbatia.
Mh Mbatia akiongoza Harambee ya ujenzi wa Bweni katika shule ya sekondari Pakula.
Mh Mbatia akizungumza na wanafunzi wanao hitimu masomo yao katika shule ya sekondari Pakula huku akihamsisha wazazi wao kuchangia ujenzi wa Bweni katika shule hiyo.
Watu mbalimbali wakichangia harambee hiyo.
Ikafika zamu ya Mh Mbatia kuchangia ambapo alitoa kiasi cha shilingi milioni 10 na ahadi ya shilingi milioni 10 yeye na familia ya Mwalmu Francis Wiliam Mbatia huku akihamasisha wanafunzi wote waliofundishwa na baba yake waone umuhimu wakuchangia shule hiyo.
Baada a mchango huo kina mama walimbeba Mbatia huku wakishangilia .
Hili ndilo Bweni linalitarajiwa kujengwa kwa ajili ya kulia chakula na kufanyia mitihani wakati wa mitihani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .