MSAFARA WA KINANA WASAFIRI KWA BAISKELI MILIMA YA USAMBARA KWENDA MKINGA,TANGA
Posted in
Matukio
No comments
Wednesday, October 1, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg'aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiongoza msafara katika safu ya milima ya Usambara kwenda Jimbo la Mkinga, Tanga.
Nyuma ya Nape ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga na nyuma ya Kinana ni Mhariri wa Habari wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Ni safari ndefu lakini yenye faraja na matumaini
Mbele ni Kinana na Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Uhuru, Seleman Jongo
Kinana mbele na kutoka kushoto ni wanahabari walio kwenye msafara huo, David John wa Majira, Seleman Jongo wa Uhuru na Said Mwishehe wa Jambo leo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :