WAKALI SISI LATIMKA NA MILIONI 5 ZA SHINDANO LA DANCE100% 2014
Posted in
Burudani
No comments
Sunday, October 5, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akitaniana na kiongozi wa kundi la”Wakali sisi”la kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto)alipokuwa akikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 5 kwa kundi hilo kama wadhamini wakuu wa shindano la Dance 100% kundi hilo liliibuka washindi katika fainali ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha The WT cha jijini Dar es Salaam kilichoshinda nafasi ya pili katika fainali ya shindano la Dance 100% 2014 likionesha umahiri wao wa kudansi katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Ambapo kundi la”WAKALI SISI”toka kiwalani jijini liliibuka na ushindi huo na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Washindi wa shindano la Dance 100% 2014 kundi la wakali sisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo na Ofisa matukio wa Basata Kurwijira Magesa (kushoto)pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kulia) mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo na kujinyakulia kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa fainali wa shindano hilo lililoandaliwa na EATV lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,ambapo kundi la”WAKALI SISI” liliibuka washindi na kunyakua kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Kinondoni, Edward Byampanju(kushoto)na Meneja uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(katikati)wakijadiliana jambo wakati wa fainali ya shindano la Dance 100% 2014.ambapo kundi la”Wakali sisi”liliibuka washindi na kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 5 na wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania,watatu toka kushoto ni Afisa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi.
Kundi la”Wakali sisi”ambao ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014,wakionesha umahiri wao wa kucheza wakati wa fainali ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuweza kujinyakulia kitita cha Tsh Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam kushuhudia mchuano mkali wa fainali ya Dance 100% ambapo kundi la Wakali sisi liliibuka na ushindi na kuweza kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :