IKULU YA TANZANIA YAHUSISHWA NA ESCROW-BBC

Posted in
No comments
Saturday, November 29, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Bunge la Tanzania hapo juzi liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tindu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.
Chanzo: BBC

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .