CESC FABREGAS NI ZAIDI YA MWANASOKA
Posted in
Michezo
No comments
Monday, December 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mchezo wa soka kwa ulimwengu huu wa tatu umekuwa ukibadilika kwa kasi kubwa huku ushindani mkubwa wa ushindani baina ya mchezaji kwa mchezaji na timu zao na timu nyingine zikizidi kuongezeka na kupanua wigo wa kushinda na kubuni mbinu za kumwangamiza adui atakayemkabili.
Hali hii inamaanisha kuwa wachezaji ambao kimsingi wanalipwa fedha nyingi sana wanalazimika kujituma mara mbili au zaidi ili kuweza kutimiza malengo ya timu zao.
Katika kudhihirisha hili wachezaji walio bora hupimwa kwa kutumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu na kinachowahukumu katika ubora au ubovu wao ni takwimu ambazo hufichua kile ambacho mchezaji anakifanya akiwa kwenye uwanja wa mazoezi na hata wakati wa mechi.
Takwimu kwenye ligi ya England zinaonyesha kuwa kiungo Mhispania wa Chelsea Cesc Fabregas ndio mchezaji aliyekimbia umbali mrefu kuliko wote katika michezo yote ambayo Chelsea imecheza msimu huu.
Takwimu zinaonyesha kuwa Cesc hadi sasa amekimbia zaidi kilomita 100 katika michezo yote aliyoichezea Chelsea kwenye ligi ya England msimu huu hali inayoonyesha kiwango kikubwa cha kujituma anapokuwa uwanjani.
Fabregas alifiisha kiwango hicho katika mchezo ambao Chelsea ilishinda 3-0 dhidi ya Tottenham jumatano iliyopita na hii ina maana kuwa katika mchezo ambao Chelsea imefungwa na Newcastle aliongeza na kufikisha zaidi ya kilometa 100.
Wachezaji wengine ambao wametimiza kilomita kia moja ya eneo walilokimbia katika katika michezo ya timu zao msimu huu ni kiungo mwingine wa Chelsea Nemanja Matic na beki wa Hull city Jake Livermore.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :