CRDB YAIPIGA 'JEKI' CHUO KIKUU CHA ST JOHN'S DODOMA

No comments
Tuesday, December 9, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred akihutubia wakati wa Mahafali ya 5 ya Chuo Kikuu cha St. John's  Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dickson Chilongani (kushoto), akikabidhiwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, mfano wa hundi na bahasha mara baada ya hotuba. Hundi hiyo ina thamani ya hundi ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada wa benki hiyo kwa Chuo Kikuu cha St. John's wakati wa Mahafali ya 5 ya chuo hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
 Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dickson Chilongani (kushoto), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred (kulia), ukiwa ni msaada wa benki hiyo kwa Chuo Kikuu cha St. John's wakati wa Mahafali ya 5 ya chuo hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili (kushoto) ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mbennah.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dickson Chilongani (kushoto), akimshuru kwa kupeana mkono na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, mara baada ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada wa benki hiyo kwa Chuo Kikuu cha St. John's wakati wa Mahafali ya 5 ya chuo hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. 
 Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imeahidi kusaidia juhudi za kukuza taaluma katika chuo hicho ili kukifanya kiwe chuo bora kutokana na mazingira ya chuo hicho kuendana na maisha ya kiroho mambo ambayo ni muhimu kwa maadili ya Taifa.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki hiyo. Philip Alfred alisema benki ya CRDB imefuatlia kwa karibu mwenendo wa chuo hicho na kujiridhisha kuwa ikiwa itatoa ushirikiano kukiendeleza  kitakuwa chuo bora nchini na katika ukanda huu wa Afrika. 

Mkurugenzi alisema amefurahishwa na muongozo unaotilia maanani na maadili kwa vijana jambo ambalo ni muhimu katika maendeleo na hatma ya Taifa na kuongeza kuwa muongozo huo uliivutia benki hiyo na kuona kuwa mafunzo yenye msingi wa kiroho yatasaidia Taifa katika uadirifu na kumcha Mungu na hilo ndilo lililonishawishi kukubali kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya. 

Alisema maendeleo ya haraka ya chuo hicho yanatokana misingi mizuri iliyowekwa ya kiroho na maadili ambayo itakiwezesha kuimarika kitaaluma kwa haraka na kulisaidia Taifa kupata wataalamu wenye uwezo katika fani mbalimbali na kuwaasa wahitimu kuachana na tamaa ya utajiri wa haraka na wizi na upokeaji rushwa wanapopata mamlaka ya uongozi.

'Hamtaweza kufanya chochote  bila ya msaada wa Mungu unapojenga nyumba lazima uweke msingi imara ambao utaifanya nyuimba kuwa imara katika mitikisiko, upepo na mafuriko', na kuongeza kuwa taaluma peke yake bila maadili ya kiroho ni bure.

Pia aliongeza kuwa kutokana na kuvutiwa na mikakati ya chuo hicho benki ya CRDB iliamua kuchangia sh. milioni 10 ambazo zitasaidia katika mipango ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi na kuahidi kuendekea kushirikiana ikiwa ni pamoja na kufungua milango kwa chuo hicho kupata mikopo ya ujenzi wa mabweni na majengo zaidi vitivo mbalimbali vya chuo hicho.

Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mbennah, alisema kila mwanachuo afahamu kuwa lazima awe na maono ya hatma ya nchi kwa hali ya baadae na kuongeza kuwa kuna upungufu wa majengo ya taaluma na malazi kwa wanachuo 688 na kuelezea kuwa hilo ni tatizo linalochangia kutofikiwa kwaalengo kwa haraka. 

Profesa Mbennah alisema chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Tanzania  kilichoanzishwa mwaka 2007 kimeendelea kuwa na matokeo mazurio katika taaluma mbalimbali na ili kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kifedha umeanzishwa mfuko maalumu ambao pamoja na matatizo mengine utasaidia kuwasomosha wanafunzi wasio na uwezo. 

Alisema Benki ya CRDB imedhihirisha ukaribu na jamii kwa kuonesha nia ya kusaidia chuo hicho ambacho kinapokea wanafunzi kutoka kila upande wa nchi hivyo ameishukuru benki hiyo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo kwa manufaa ya Taifa.

Viongozi wengine waliohudhuria mahafali hayo ni Askofu Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dodoma, Dickson Chilongani, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Dodoma Rehema Hamis, Meneja wa Tawi la UDOM, Chabu Mishwaro Askofu Mkuu Mstaafu Dornald Mtetemela na vi.ngozi wengine.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .